Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ikishirikiana na wadau wake
kuanzia kesho wanatarajia kuanza kutoa huduma kwa saa 24, siku saba za
wiki, mwaka mzima bila kupumzika.
Ofisa Uhusiano wa TPA, Janeth Zurangi alisema
uamuzi huo ambao unakusudia kuongeza ufanisi wa bandari hiyo, umefikiwa
baada ya wadau mbalimbali kutia saini mikataba ya utekelezaji kazi hiyo.
Zurangi alisema ingawa kulikuwapo mabishano kuhusu
vipengele kadhaa ndani ya mkataba huo, wadau wote walikubali kuanza
kutoa huduma kila siku kwa saa 24 kuanzia Machi Mosi.
“Mwezi ujao utaratibu huo utaanza na tunatarajia
utakuwa na mafanikio makubwa. Hivi sasa mteja anaweza kuchelewa kuchukua
mzigo kwa sababu baadhi ya wadau hawajasaini vibali husika,” alisema.
Oktoba 14 mwaka jana, Waziri wa Uchukuzi, Dk
Harrison Mwakyembe aliwataka wadau wengine wanaofanya kazi na TPA
kuanzisha utaratibu wa kufanya kazi kila siku, kwa kile alichoeleza
kutofanya hivyo kunakwamisha kasi ya uondoaji mizigo bandarini.
Dk Mwakyembe alinukuliwa akisema: “Bandari
wanafanya kazi saa 24 kwa siku saba za wiki bila kupumzika, lakini
wenzetu wa TRA wao sikukuu na siku za mwisho wa juma wanalala hali hii
inaturudisha nyuma kimapato.” Baadhi ya wadao waliosaini mkataba huo ni
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Chama cha Wakala wa Forodha na
Uondoshaji Shehena Tanzania (Taffa).
Chanzo ;Mwananchi
Chanzo ;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment