Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umeanza mkakati wa kupima afya za Watanzania bila malipo nchini nzima.
Mfuko huo ambao uko nchi nzima,umekuwa ukitoa
huduma za upimaji huo, ambapo mpaka sasa wananchi wa Mikoa ya Dar es
Salaam, Arusha, Kilimanjaro na Zanzibar wamenufaika na mpango huo.
Meneja Mfuko wa Ilala, Christopher Mapunda alitaja
magonjwa yatakayopimwa na wahusika kupewa ushauri wa kitaalamu katika
mpango huo kuwa ni magonjwa yasiyoambukizwa ikiwamo kisukari, shinikizo
la damu, uzito na urefu.a
Meneja huyo alikuwa akizungumza wakati wadau wa
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), waliofika katika banda
la NHIF kwa ajili ya kupima afya zao wakati wa mkutano wa mwaka wa mfuko
huo,
Mkurugenzi huyo alisema lengo la mpango huo ni
kusaidia jamii kujiepusha na magonjwa hayo kwa sababu watakuwa wakitoa
elimu kwa kuhusu afya kwa wahusika wote ambao afya zao zimeonekana kuwa
na matatizo
“Hii itasaidia kutoa utaratibu wa kula na kufanya
mazoezi, ili kuuweka mwili kwenye hali nzuri kiafya kwa kuwa mfuko
unaendesha mpango huo ili kuwawezesha wananchi wajue umuhimu wa kupima
afya zao na shughuli za NHIF,” alisisitiza.
Mkurugenzi huyo aliwataka wananchi wote kujiunga
na mfuko huo, kwa kuwa gharama za matibabu kwa sasa zipo juu na kwamba
siyo rahisi kwa mwananchi wa kawaida kuweza kuzimudu kwa wakati mmoja.
“Ieleweke wazi kwamba kwa sasa gharama za matibabu
ni ghali sana, siyo rahisi kuzimudu kwa wakati mmoja, lakini ukiwa na
NHIF kadi yako ya matibabu tayari inakuhakikishia kupata matibabu muda
wowote’alisema
Awali baadhi ya wananchi waliopata huduma hiyo,
waliupongeza mfuko huo kwa kuwasaidia kujua afya zao, huku wakisisitiza
kwamba bila afya bora hakuna maendeleo endelevu katika jamii.
Chanzo;mwananchi
Chanzo;mwananchi
0 comments:
Post a Comment