JAJI
mkuu mstaafu Raymond Mwaikasu amependekeza Viongozi wa jeshi la
magereza waingizwe katika rasimu ya katiba kwa sababu ni watekelezaji
wa sheria za nchi husika hivyo viongozi wakuu wa magereza
washirikishe katika kamati ya ulinzi na usalama wa taifa kwa sababu ni
sehemu ya nchi washirika.
Akizungumza
katika warsha iliyofanyika mjini Iringa yenye lengo la
kuwajengea uelewa wa katiba pamoja na mchakato wa marekebisho ya katiba
kwa wananchi waishio wilaya ya Iringa vijijini, alisema kuwa viongozi
wa Magereza waingizwe katika kamati ya ulinzi na usalama wa Taifa ili
kuweza kutoa taarifa kwa kamati juu ya yanayotokea gerezani na
wanayokabiliana nayo katika magereza.
Kwa
upande wake MKurugenzi mkuu John Msika alisema kuwa jeshi la magereza
halijatajwa kama ni sehemu ya muungano hivyo halimtambui katika
kuidhinisha adhabu.
“Mkuu wa jeshi la magereza aidhinishe kama mmoja wa wanakamati na mjumbe katika kamati kuu ya ulinzi na usalama “alisema Msika
Naye
mkurugenzi wa mafunzo na utafiti Erick Nyato alisema kuwa Muundo wa
serikali tatu utahimiza na kujari maadili na miiko ya viongozi wa umma
kupunguza mamlaka ya Rais katka uteuzi wa viongozi mbali mbali.
Suala
la serikali tatu sio kuvunja amani hili ni suala la uongozi kama
itashindikana ni kubadilisha uongozi kwa sababu ni maamuzi yetu wenyewe
wananchi .
Michuzi Media Group
Michuzi Media Group
0 comments:
Post a Comment