Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais,Jakaya Kikwete.
Kificho alisema jana kuwa kamati hiyo ilifanya kazi kuanzia Februari 19 hadi 23, mwaka huu, kwa kuangalia mambo matano ili kujenga hoja ya kupeleka serikalini kwa ajili ya kupata majibu ya hoja ya wajumbe.
Alisema kamati hiyo yenye wajumbe sita iliangalia mambo matano ambayo ni hali ya gharama za maisha Dodoma, aina ya wajumbe walioteuliwa na kuwianisha na pato la kila mjumbe kabla ya kuteuliwa kuwa mjumbe, kuangalia sheria kuhusu taratibu za posho, uwazi wa jinsi posho zinavyotolewa, ulinganisho wa malipo kwa kuzingatia aina ya wajumbe wote.
“Tangu Februari 19 hadi 23, mwaka huu, kamati imetafakari maoni yenu kwa upana zaidi na kuzingatia masharti yaliyotolewa, kama inavyojulikana masharti ya mjumbe yapo kwenye mamlaka iliyomteua...kamati imewasilisha mapendekezo yake kwenye mamlaka hiyo,” alisema.
Aidha, alisema baada ya kamati kujiridhisha imewasilisha mapendekezo kwenye mamlaka husika na kutoa mapendekezo yao.
Aliwasihi wajumbe hao kuwa na subira wakati wanasubiri majibu ya mapendekezo hayo juu ya hoja wa wajumbe. “Nasi ni wadau wa jambo hili tusubiri mamlaka husika zitoe mapendekezo ya suala hilo ili kuhakikisha shughuli za Bunge zinaendelea kama kawaida kwa manufaa ya Watanzania,” alisema.
Suala la posho kwa wajumbe hao liliibuliwa ndani ya ukumbi huo Februari 19, mwaka huu na mjumbe, Richard Ndassa, ambaye alidai baada ya kusoma kwenye kitabu cha masharti ya kazi kilichoainisha stahili ya posho za kujikumu na kikao.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment