Home » » Kamati Kuu Chadema kukutana kwa dharura leo

Kamati Kuu Chadema kukutana kwa dharura leo

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
 
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), leo inatarajia kufanya kikao cha dharura  jijini Dar es Salaam kujadili na kufanya uteuzi wa mwisho wa jina la mgombea ubunge wa Chadema katika uchaguzi mdogo wa  wa Jimbo la Kalenga mkoani Iringa.
Hatua hiyo imekuja baada ya Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) kutangaza kuwa uchaguzi wa ubunge katika jimbo hilo utafanyika Machi 16, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho kwa vyombo vya habari, Chadema kitafanya uteuzi wa mwisho baada ya mchakato wa ndani wa kumpata mgombea ubunge wake wa jimbo hilo kuwa umepitia hatua za awali.

Hatua hizo  ni pamoja na watu wote wenye nia ya kugombea kuchukua fomu za uteuzi wa ndani tangu Februari 5 hadi 10, mwaka huu.

" Kama ilivyoelezwa kwa umma kupitia vyombo vya habari, Februari 6, mwaka huu, fomu hizo zilitolewa katika maeneo matatu, Ofisi za Makao Makuu ya Chama, Dar es Salaam, Ofisi za Jimbo la Kalenga na kwenye tovuti ya chama, ambayo ni; www.chadema.or.tz," ilieleza sehemu ya taarifa ya chama hicho.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,  wanachama wa chama hicho 16 walichukua fomu za kuwania uteuzi huo na kwamba hadi siku ya mwisho,  13 walirejesha kupita kwenye mchakato wa kura za maoni, zilizofanyika Februari 12, mwaka huu.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo na Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa kufariki dunia.
CHANZO: NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa