Home » » Bunge likumbuke sekta ya afya

Bunge likumbuke sekta ya afya

Dar es Salaam.Muunganiko wa wadau wa afya umeitaka Serikali na wajumbe wa Bunge la Katiba kuweka suala afya kama mojawapo ya haki za msingi za Watanzania.
Na kwa sababu hiyo, wameshauri Bunge kuhakikisha linasimamia mabadiliko kwa masilahi ya taifa.
Akizungumza wakati wa kutoa tamko hilo la wadau wa afya lililohusisha asasi ya Sikika, Chama cha Madaktari(MAT), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Chama cha Afya ya Jamii, Mkuu wa Program ya Sikika Josephat Mshighati alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya kuona Rasimu ya Katiba haijazungumzia kwa undani kuhusiana na suala la afya.
Alisema licha ya kukutana na kupeleka maoni yao kwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutaka afya iwe mojawapo ya haki za msingi za Mtanzania ,suala hilo halikuzingatiwa ingawa lina umuhimu mkubwa kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi.
“Tumeona rasimu imegusia kuhusiana na suala la afya, lakini hakuna kifungu kilichojadili kwa undani hivyo jambo hili linaonekana kama kitu cha kawaida.”
Chanzo;Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa