Home » » Mkurugenzi kortini akidaiwa kuua watu wanne

Mkurugenzi kortini akidaiwa kuua watu wanne

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mkurungenzi wa zamani wa Manispaa ya Ilala jijini Dar- es- Salaam, Gabriel Fuime (61).
 
Mkurungenzi  wa zamani wa Manispaa ya Ilala jijini Dar- es- Salaam, Gabriel Fuime (61), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu  mashitaka manne ya mauaji ya watu wanne.
Fuime alisomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mmbando, ikidaiwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Bernad Kongola , kuwa Machi 29, 2013 katika  mtaa wa Indira Ghadh Dar –es- Salaam, mshtakiwa  alimuua kwa makusudi Gabriel Kamwela.

Kongola alidai katika shitaka la pili,  akiwa mtaani hapo kwa mara nyingine  mshtakiwa huyo  alimuua Philipo Kusimala na katika shitaka la tatu na la nne, Fuime  anadaiwa kuwaua Bethod Mwanengule na Zahda Kanji.

Kwa mujibu wa Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai, Fuime hakutakiwa kujibu chochote hadi upelelezi wa kesi yake utakapokamilika na kuhamishiwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Upande wa Jamhuri ulieleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe ya kutaja tena. Hakimu Mmbando alisema kesi hiyo itatajwa Machi 5 mwaka huu na mshtakiwa kurudishwa mahabusu.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa