MTOTO
wa kike mwenye umri wa miaka nane mkazi wa Muungano Tungi Kigamboni,
wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, amenajisiwa hadi kuzirai, kisha
kutelekezwa pembezoni mwa makaburi eneo la Magogoni .
Akizungumzia
tukio hilo akiwa hospitalini Temeke anakoendelea na matibabu, huku akiwa
na majeraha sehemu mbalimbali za mwili ikiwa ni pamoja na usoni, mtoto
huyo (jina linahifadhiwa) alisema alifanyiwa unyama huo na kijana ambaye
hamfahamu.
Alisema wakati akitoka shuleni alitokea kijana huyo akiwa
na baiskeli, ambapo alimwambia apande ili amsaidie kumrudisha nyumbani.
Alisema
baada ya kupanda baiskeli hiyo kijana huyo alimpeleka eneo ambalo
halifahamu na kumfanyia unyama huo. Akizungumzia tukio hilo, mama wa
mtoto huyo (jina tunalo) alisema baada ya kuona mtoto anachelewa kurudi
nyumbani alitoa taarifa kwa mume wake na ndipo walianza kumtafuta.
Alisema
walitoa taarifa Kituo cha Polisi Kigamboni na ilipofika saa 12 jioni
mtoto huyo alikutwa na wasamaria wema akiwa amepoteza fahamu eneo la
makaburi ya Magogoni ambapo alifikishwa kituo hicho akiwa hajitambui.
Aliongeza
kuwa mtoto huyo alipata majeraha sehemu mbalimbali za mwili, hasa
katika paji lake la uso ambapo inaonekana alikwaruzwa na na kucha na
kupata jeraha sehemu ya shavuni.
Kwa upande wa Mjumbe wa Serikali ya
Mtaa wa Tungi, Farida Jumbe, alisema hatua mbalimbali zilichukuliwa
kumsaidia mtoto huyo kwani baada ya kufikishwa Polisi Kigamboni alipewa
PF3 kwa ajili ya kwenda kutibiwa hospitali.
"Hadi sasa anaendelea na
matibabu Hospitali ya Temeke," alisema. Naye Ofisa Jamii wa Tungi,
alisema mara nyingi matukio kama haya yanaweza kutokea katika maeneo
mengi ya vichaka.
Alishauri juhudi zifanyike ili kupunguza vichaka vinavyotumika kufanyia vitendo hivyo.
Juhudi za kumpata Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke kuzungumzia tukio hilo, ziligonga mwamba
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment