UGONJWA
wa saratani umezidi kuongezeka kwa kasi nchini kila mwaka ambapo
wagonjwa wapya wa saratani wanaogundulika ni 44,000 na kati ya hao
wanaofariki 35,000.
Takwimu hizo zimetolewa na Serikali Dar es
Salaam jana wakati wa maadhimisho ya siku ya Saratani Duniani.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii, Dkt Seif Rashid, alisema tatizo hilo kwa sasa ni kubwa kwa taifa
hasa kutokana na wagonjwa hao kufika katika vituo vya tiba wakati
ugonjwa huo ukiwa kiwango cha juu.
Alisema wengi wanafika hospitali ugonjwa huo ukiwa umefikia hatua ya tatu au nne, hivyo inakuwa vigumu kupona.
“Saratani
inayoongoza zaidi kwa wanaume ni saratani ya Kaposi na saratani ya tezi
dume, huku kwa upande wa wanawake saratani ya shingo ya kizazi ikiwa
inaongoza," alisema.
Alisema takwimu za wagonjwa zimekuwa
zikiongezeka siku hadi siku, hali inayosababisha Serikali kuchukua hatua
ya kukabiliana na tatizo hilo kwa kutoa elimu ya kutosha na kuboresha
sekta ya tiba kwa wagonjwa.
Dkt. Rashid alisema kwa miaka mingi
matibabu ya saratani yalikuwa yakitolewa katika Taasisi ya Saratani
Ocean Road na ili kuboresha huduma Serikali imeanzisha kutoa tiba hizo
katika Hospitali ya Bugando. Alisema matibabu hayo yanatarajiwa
kuanzishwa pia kwenye hospitali za Rufaa KCMC na Mbeya.
Alisema
Serikali imejipanga kufanya juhudi kuhakikisha fedha, vifaa tiba na dawa
za kukabiliana na ugonjwa wa saratani vinapatikana ili kuinua hali ya
afya ya jamii.
Akizungumzia uhaba wa madaktari, alisema juhudi za
dhati zinafanyika ambapo kwa mwaka huu Serikali imegharamia mafunzo kwa
wataalamu tisa ambapo pia wanatarajia kuongeza wengine 100 hadi 120 ili
kukabiliana na tatizo hili.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Saratani Ocean Road, Twalib Ngoma, alisema changamoto iliyopo katika
kukabiliana na ugonjwa huo ni uhaba wa vifaa.
Alitoa mfano akisema
mashine za mionzi ambazo zinahitajika ni tisa, lakini ambazo
zimepatikana ni mbili hali inayosababisha wa gonjwa kuchelewa kupewa
matibabu.
Aliitaka jamii kuelewa kuwa saratani ya shingo ya kizazi
inasababishwa zaidi na kirusi aina ya Human Abnormal ambapo Tanzania ipo
katika mchakato wa kupata chanjo yake.
Alitaja baadhi ya sababu zinazochangia saratani kwa wanawakeni kufanya mapenzi na wanaume zaidi ya mmoja bila kinga.
Sababu
nyingine ni uvutaji wa tumbaku ukichangia ugonjwa wa saratani kwa
asilimia 40 na tafiti za Benki ya Dunia zinasema kuwa kila dola moja
ambayo mapato yake kwa taifa yanatokana na biashara ya Tumbaku
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment