Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D.
Yambesi akifungua mkutano wa wadau kuhusu Mikataba ya Utendaji Kazi
katika Taasisi za Umma katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Mkutano huo uliandaliwa mahsusi ili wadau waweze kufahamu mambo muhimu
juu ya Mfumo wa Mikataba ya Utendaji Kazi hususan chimbuko, maana na
faida zake, mambo ya msingi yatakayofanikisha utekelezaji wa mfumo huo,
fomu ya mkataba wa utendaji kazi na vipengele vyake, vigezo vya upimaji
wa utendaji kazi wa taasisi, wahusika wa mikataba na utaratibu wake;
utaratibu wa kutoa taarifa za mikataba ya utendaji kazi, utaratibu wa
kutathmini mikataba ya utendaji kazi; utaratibu wa kushindanisha Taasisi
za Umma; na Taasisi zinazopendekezwa kuingia katika Mikataba ya
Utendaji Kazi . Sambamba na hilo wadau walipata fursa ya kutoa maoni,
ushauri na mapendekezo juu ya mfumo wa Mikataba ya Utendaji Kazi, na
namna bora ya kuitekeleza katika Taasisi za Umma. Wadau walioshiriki
mkutano huo ni pamoja na watendaji na watendaji wakuu wastaafu katika
Taasisi za Umma wakiwemo Makatibu Wakuu wastaafu, watendaji wakuu wa
Asasi za Kiraia (AZAKI), wanataaluma kutoka vyuo vya Elimu ya juu,
wawakilishi kutoka katika sekta binafsi na Washauri waelekezi
Wanaojitegemea.
Sehemu
ya baadhi ya wadau walioalikwa katika Mkutano kuhusu Mikataba ya
Utendaji Kazi katika Taasisi za Umma wakimsikiliza mgeni rasmi Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D.
Yambesi (hayupo pichani).
Wadau
walioshiriki mkutano kuhusu Mikataba ya Utendaji Kazi katika Taasisi za
Umma wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi (wa sita
kutoka kulia mstari wa mbele), kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Bw. HAB
Mkwizu na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri
Kazi Bw. Mick Kiliba.
0 comments:
Post a Comment