Waziri
wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa Na Serikali za Mitaa Hawa
Ghasia akieleza kwa waandishi wa Habari(Hawapo Pichani) kuhusu Mikakati
Madhubuti ya ukusanyaji mapato na Matumizi bora ya fedha zinazotolewa na
Serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Mikoa na Halmashauri
zote nchini, wakati wa Mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es
Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah
Mwambene.
Baadhi
ya waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano wa Waziri wa Nchi,Ofisi ya
Waziri Mkuu Tawala za Mikoa Na Serikali za Mitaa Hawa Ghasia, Katika
Ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Silayo.
MAELEZO YA WAZIRI WA NCHI OWM-TAMISEMI KWA
VYOMBO YA HABARI KUHUSU USIMAMIZI NA UDHIBITI WA FEDHA KATIKA MAMLAKA ZA
SERIKALI ZA MITAA
1.
UTANGULIZI
Usimamizi wa fedha katika ngazi ya Mamlaka
za Serikali za Mitaa unaongozwa na Sheria, Kanuni na Taratibu mbalimbali ambazo
ni pamoja na:-
i.
Sheria
ya Fedha ya Mamlaka za Serikali za Mitaa Sura ya 290 ambayo inaainisha Mamlaka na taratibu
mbalimbali zinazohusu Usimamizi wa fedha kwenye Mamlaka za Serikali za
Mitaa.
ii.
Sheria
ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004 na kanuni zake za Mwaka 2005.
iii. Kanuni za Usimamizi wa fedha katika Mamlaka za Serikali
za Mitaa ambazo ni Mwongozo katika utaratibu na Usimamizi wa fedha kama
ifuatavyo:-
–
Memoranda
ya usimamizi wa fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ya mwaka 1997 kama
ilivyorekebishwa mwaka 2009 (Local Government Financial Memorandum),
– Kanuni za Kudumu za Halmashauri,
– Kanuni za uanzishaji na uendeshaji
wa Bodi za Zabuni katika Mamlaka za Serikali za Mitaa za mwaka 2007,
–
Mwongozo
wa uhasibu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (Local Authority Accounting Manual) wa mwaka 2009,
–
Mwongozo
wa ukaguzi wa ndani wa mwaka 2005, na
–
Mwongozo
wa mipango na bajeti unaotolewa kila mwaka.
Usimamizi wa Sheria na
Kanuni tajwa hapo juu ni nguzo muhimu katika kuimarisha utawala bora katika
usimamizi wa fedha. Katika masuala haya, Ofisi ya Waziri
Mkuu-TAMISEMI inasimamia kwa karibu kuhakikisha Mamlaka za Serikali za Mitaa
zinatekeleza majukumu yake inavyopaswa.
Usimamizi
wa fedha katika ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa umegawanyika katika
maeneo makuu yafuatayo:-
1. Vyanzo
vya fedha (Financing Resources) - fedha za kuendeshea shughuli mbalimbali za
Halmashauri;
2. Utumiaji
wa fedha (Uses of Finance) - matumizi ya fedha zilizokusanywa na kupokelewa; na
3. Udhibiti wa rasilimali
(Controlling of Resources) - Namna ya kudhibiti ubadhirifu au upotevu wa aina
yeyote ile unaohusu rasilimali za Serikali za Mitaa.
2.
VYANZO
VYA FEDHA ZA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA
Wajibu wa msingi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ni kutoa huduma za msingi
za kijamii na kusimamia Utawala Bora. Gharama za utoaji huduma hizo unatokana
na mapato ya kodi, ushuru na ada mbalimbali, ruzuku toka Serikali Kuu, pamoja
na misaada toka kwa Washirika wa Maendeleo na Mikopo kutoka kwenye Taasisi
mbalimbali za fedha. Hivyo vyanzo vya fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa kisheria vimegawanyika katika makundi matatu yafuatayo:-
2.1
Mapato ya Ndani (Own Source
Revenue).
Kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa Sura ya 290 Kifungu cha 6, 7, 8 na 9
vyanzo mbalimbali vya mapato vimeainishwa kwa Halmashauri za Jiji, Miji, Wilaya
na Vijiji. Vyanzo vilivyotajwa katika Vifungu hivyo vinatoa nafasi kwa Mamlaka
za Serikali za Mitaa husika kutunga Sheria Ndogo zitakazowezesha Mamlaka hizo
kukusanya mapato kutokana na vyanzo hivyo. Miongoni mwa mapato hayo ni ushuru
wa leseni, ushuru wa kodi ya huduma, ushuru wa mazao, Kodi ya majengo, ushuru
wa magulio na masoko na ada za kuegesha magari.
Mapato ya Halmashauri kutoka vyanzo vyake vya ndani
kwa miaka nane (2005 -2013) iliyopita yanaonesha kuwa makisio na makusanyo ya
mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa yamekuwa yanaongezeka. Mfano, kwa miaka
mitano iliyopita yaani Mwaka 2008/09 makisio yalikuwa ni shilingi bilioni 107.6 na makusanyo halisi yalikuwa
shilingi bilioni 93.7 ambayo ni asilimia 87 ya makadirio. Kwa mwaka wa
fedha 2009/10 makadirio yalikuwa shilingi bilioni
130.9 ambapo makusanyo yalikuwa shilingi bilioni 117.8 sawa na asilimia
90 ya makadirio. Mapato haya yameendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka ambapo
kufikia Mwaka 2012/13 makadirio yalikuwa kukusanya shilingi bilioni 328.4 na makusanyo yalikuwa
shilingi bilioni 240.9 sawa na asilimia 73.3. Ongezeko la makadirio
kwa miaka hii nane yaani kutoka 2005/06 hadi 2012/13 ni sawa na asilimia 512.9
wakati makusanyo yameongezeka kwa asilimia
389. Mtiririko wa mapato hayo kwa kipindi hicho ni kama inavyoonekana
katika jedwali lifuatalo:
|
Mwenendo Wa Mapato ya Ndani
ya Halmashauri kuanzia Mwaka 2005/6 Hadi Mwaka 2012/13
|
|||
|
Mwaka
|
Makadirio
|
Makusanyo
Halisi
|
% Ya
Makusanyo
|
|
2005/06
|
53,593,591,293
|
49,291,049,660
|
92.0
|
|
2006/07
|
63,385,237,737
|
61,411,259,961
|
96.9
|
|
2007/08
|
80,136,598,991
|
79,770,210,999
|
99.5
|
|
2008/09
|
107,628,203,817
|
93,752,903,592
|
87.1
|
|
2009/10
|
130,887,328,313
|
117,783,506,345
|
90.0
|
|
2010/11
|
175,084,789,727
|
158,279,374,601
|
90.4
|
|
2011/12
|
310,962,562,609
|
195,524,503,634
|
62.9
|
|
2012/13
|
328,450,131,918
|
240,908,504,656
|
73.3
|
Mwenendo wa ukusanyaji wa mapato unaonesha kuwa Mamlaka
za Serikali za Mitaa zimeendelea kujitahidi katika ukusanyaji. Hata hivyo
Serikali inaendelea kuzijengea uwezo Halmashauri ili ziweze kufikia malengo ya
ukusanyaji waliojiwekea. Kwa sasa Serikali kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo
imeendelea kufanya yafuatayo:-
·
OWM –
TAMISEMI imekamilisha utafiti wa vyanzo vya mapato katika Mamlaka za Serikali
za Mitaa 30 (za majaribio) katika kipindi cha Julai – Septemba, 2013, ambapo
vyanzo mbalimbali vipya vinavyoweza kutozwa Kodi vimeibuliwa kama Kodi ya
majengo kwa Halmashauri za Wilaya, Ushuru wa Mifugo, Ushuru wa Minara ya Simu,
Ushuru wa nyumba za kulala wageni uliofutwa awali nk. Maeneo hayo yatapanua
wigo wa mapato wa Halmashauri pamoja na maeneo yanayotakiwa kufanyiwa
marekebisho ya Kisheria (Sheria ya Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa ya
mwaka 1982) ili kuongeza wigo wa mapato. Vile vile, utafiti huo umeangalia njia
za kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato pamoja na njia za malipo rahisi
ili kupunguza kero na umbali kwa walipaji hasa katika kulipa kupitia teknolojia
rahisi za malipo kwa kutumia M- Pesa, Tigo – Pesa, Max- Malipo, n.k.
·
OWM-TAMISEMI
kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara imerudisha Ada za Leseni za
Biashara kuanzia mwezi Julai, 2013 ili kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa
kuongeza vyanzo vya ukusanyaji wa mapato.
·
OWM-TAMISEMI
itaendelea kusimamia kikamilifu Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuhakikisha
zinakusanya mapato yake ya ndani ipasavyo ikiwa ni pamoja na kutumia mifumo ya
kielektroniki ya usimamizi wa mapato yaani “Local Government Revenue Collection
System (LGRCS)” na “i-TAX” kwa lengo
la kuboresha usimamizi na udhibiti wa mapato ya ndani ya Halmashauri na kuhakikisha
mapato haya yanatumika inavyopaswa.
·
Halmashauri zimeendelea
kuchukua hatua za Kisheria kwa Mawakala wote ambao hawajawasilisha makusanyo ya
mapato pamoja na wale wote wanaokwepa kulipa ushuru kulingana na taratibu
zilizopo. Mfano mwaka 2011/12 Mawakala 35 wa ukusanyaji mapato katika Halmashauri
mbalimbali wamefikishwa Mahakamani kwa kutowasilisha makusanyo kulingana na
makubaliano.
·
OWM-TAMISEMI
imeendelea kuzielekeza Halmashauri zote nchini kubuni vyanzo vipya vya mapato
kulingana na uwezo na uchumi wa maeneo yao ili kuwaongezea kipato. Kadhalika,
maelekezo yametolewa kwa Halmashauri kuhakikisha kodi zinazotozwa sasa
zinakusanywa kikamilifu na kwamba mbinu za ukusanyaji zinaboreshwa ili kuongeza
mapato. Mikoa nayo imeagizwa kutekeleza jukumu lake la msingi la kuzisaidia na
kusimamia Halmashauri ipasavyo ikiwemo eneo la ubunifu wa vyanzo vya mapato.
2.2
Ruzuku toka Serikalini na kwa
Washirika wa Maendeleo
Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mujibu wa Kifungu
cha 10 cha Sheria ya Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa zinapaswa kupokea
ruzuku toka Serikali Kuu ili kulipia gharama za utoaji wa huduma mbalimbali
kama Afya, Elimu, Kilimo, Barabara na maji. Ruzuku hii ni kwa ajili ya Matumizi
ya Kawaida, Mishahara na Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo. Suala la kupeleka fedha za ruzuku katika MSM linategemea
upatikanaji wa fedha za makusanyo ya ndani ya Serikali na kutoka kwa Washirika
wa Maendeleo. Pale ambapo Serikali Kuu imekusanya mapato kidogo kutoka katika
vyanzo hivyo, upelekaji wa fedha katika MSM nao huwa mdogo.
2.3
Mikopo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa
Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mujibu wa Kifungu
cha 11 cha Sheria ya Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa Sura 290 zina fursa ya kukopa kutoka katika Taasisi za
fedha na Mabenki ili kupata fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya
maendeleo. Hadi kufikia Juni, 2013 Halmashauri zipatazo 21 zimepatiwa Mikopo
kupitia Taasisi za binafsi za Fedha. Pia Kifungu na 12 cha Sheria hiyo kinatoa
nafasi kwa Halmashauri kutumia fedha zaidi ya akiba iliyopo Benki kwa kupata
kibali cha Waziri mwenye Dhamana ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Kadhalika, Mamlaka za Serikali za Mitaa zinaruhusiwa
kukopa fedha kutoka Bodi ya Mikopo ya
Serikali za Mitaa. Hadi kufikia Septemba, 2013 Bodi ya Mikopo ya Serikali
za Mitaa imeweza kutoa mikopo ya jumla ya Shs. 6,935,736,734/=. Aidha, zipo
Halmashauri zilizowasilisha maombi ya mikopo ambayo yanaendelea kushughulikiwa
ili yaweze kupata vibali vya kukopa. OWM – TAMISEMI imendaa Mwongozo maalum
unaozielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa kuzingatia taratibu muhimu za
kufuatwa kabla ya kuwasilisha maombi ya Vibali vya mikopo.
3.
UTUMIAJI
WA FEDHA
Usimamizi katika matumizi ya fedha za Umma
unaanzia katika utengenezaji wa bajeti. Serikali huandaa Mwongozo wa namna ya
kuandaa bajeti kila mwaka ambapo Mamlaka za Serikali za Mitaa huutumia kuandaa
bajeti zao kwa kuzingatia ushirikishwaji wa jamii katika kuibua Miradi ya Maendeleo
kulingana na mahitaji ya eneo husika. Katika Usimamizi wa Mapato na Matumizi ya
Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa, Kanuni za Usimamizi wa Fedha wa Mamlaka za
Serikali za Mitaa (LAFM, 2009) zimeainisha wajibu na majukumu ya makundi
mbalimbali ya Viongozi na Watendaji katika Mamlaka hizo ambao wana wajibu wa
kusimamia matumizi hayo kama ifuatavyo:
3.1
Waziri mwenye Dhamana ya
Mamlaka za Serikali za Mitaa
Kuhakisha kuwa upo usimamizi madhubuti wa mapato na matumizi katika Mamlaka
za Serikali za Mitaa; kuwezesha kuwepo kwa usalama wa fedha kwa ajili ya
shughuli za Mamlaka za Serikali za Mitaa na kuhakikisha kuwa Mamlaka za
Serikali za Mitaa zinatekeleza shughuli zake kwa mujibu wa mipango na bajeti
ikiwemo kuziwezesha ili ziweze
kutoa huduma bora kwa wananchi. Kadhalika kuchukua hatua stahiki kwa Watendaji
watakaobainika kufanya ubadhirifu wa mali ya umma.
3.2
Mkuu wa Mkoa.
Kuhakiki na
kupitia taarifa za mapato na matumizi ikiwemo zile za utekelezaji wa miradi ya
maendeleo za kila robo mwaka; kutoa ushauri katika mipango na bajeti za
Halmashauri; kupitia taarifa za Mkaguzi wa Ndani za kila robo mwaka; kupitia
taarifa za Kamati za Ukaguzi (Audit Committee),
kufanya ukaguzi maalum wa masuala ya fedha na kuchukua hatua stahiki kulingana
na Sheria, Taratibu na Kanuni zilizopo.
3.3
Baraza la Madiwani.
Baraza la Madiwani
lina wajibu wa kutoa maamuzi katika masuala yote ya usimamizi wa utekelezaji wa
shughuli za Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo kuidhinisha mipango na bajeti
za Halmashauri; kujadiliana, kukubali au kukataa mapendekezo ya taarifa za
utekelezaji zilizowasilishwa na Kamati za Kudumu pamoja na kuchukua hatua
stahiki kwa watumishi walioenda kinyume na Sheria.
3.4
Kamati ya Fedha na Uongozi.
Kudhibiti na Kusimamia Mapato na Matumizi ya
Halmashauri kwa kupitia taarifa za mapato na matumizi ya kila mwezi; taarifa za
utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya kila robo mwaka; taarifa za Mkaguzi wa
ndani na zile za Kamati ya Ukaguzi. Pia kuidhinisha mipango na bajeti ya mwaka
ya Halmashauri; kupitia taarifa za Bodi ya Zabuni; kupitia taarifa za Kitengo
cha Manunuzi cha Halmashauri (PMU), na kusimamia
uwasilishaji wa taarifa za mwisho wa
mwaka wa fedha kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
3.5
Menejimenti ya Halmashauri.
Mkurugenzi ndiye Afisa Masuuli wa Halmashauri kwa
hiyo kwa kushirikiana na Wakuu wa Idara, anao wajibu wa kuhakikisha kuwa Halmashauri
ina mfumo rasmi na wa kuridhisha wa usimamizi wa fedha; Sheria, Kanuni na Miongozo
ya Usimamizi wa fedha inafuatwa kwa ukamilifu na Idara zote katika utekelezaji
wa shughuli za Halmashauri; kusimamia Mapato, Matumizi, Mali na Madeni yote ya
Halmashauri; kujibu Hoja za ukaguzi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali, Mkaguzi wa Ndani na Kamati zozote za Ukaguzi kwa wakati na ukamilifu;
pamoja na kuhakikisha kuwa Madiwani wanapewa taarifa zinazohusu masuala ya
fedha kwa wakati.
Katika kutekeleza majukumu haya ya usimamizi kwa
upande wa matumizi, zipo taarifa mbalimbali zinazoandaliwa katika ngazi zote
zinazoonesha mapato yaliyopatikana na namna fedha hizo zilivyotumika. Lengo ni
kuona fedha hizi zimetumika katika maeneo yaliyokusudiwa na kwamba thamani ya
fedha hizo inaonekana ili hatimaye kutoa huduma za msingi kwa wananchi.
Taarifa hizi huonesha mapato na matumizi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa
ikiwemo miradi ya maendeleo na hupitiwa na Vikao na Kamati mbalimbali zikiwemo; Baraza
la Madiwani, Kamati ya Huduma za Jamii, Kamati ya Huduma za Kiuchumi na Kamati ya Fedha
na Uongozi/Mipango).
Kamati ya Fedha na Uongozi inakutana kila
mwezi. Baraza la Madiwani na Kamati za Huduma za Jamii na Huduma za Kiuchumi
hukutana angalau mara moja kila robo mwaka. Kamati hizi hujadili na kujiridhisha kama taarifa hizi ni sahihi
na kama zinawakilisha matakwa ya wananchi kwa mujibu wa mipango na bajeti za
kila mwaka. Matakwa ya wananchi yanapatikana kwa kuwahusisha na kuwashirikisha
katika Vikao vya kupanga na kuamua vipaumbele vinavyotokana na mazingira,
nyakati na mahitaji waliyonayo.
Taarifa hizi
hupelekwa ngazi ya Mkoa ambapo huthibitishwa usahihi wake, kuunganishwa na
kuwasilishwa OWM-TAMISEMI kwa uchambuzi na kutoa maamuzi mbalimbali.
4.
UDHIBITI
WA RASILIMALI
Serikali inawajibika kwa wananchi ambao ni
walipa kodi na Washiriki wa Maendeleo wanaotupatia misaada kuhakikisha kuwa
fedha zao zinatumika kwa maendeleo ya nchi na hazifujwi.
4.1
Mfumo wa Usimamizi wa Fedha (Epicor 9.05)
Ili kuhakikisha kunakuwepo matumizi sahihi ya fedha na
utoaji taarifa, Serikali ilianzisha mfumo wa kudhibiti matumizi ya fedha yaani “Intergrated Financial Management System (IFMS)”. Katika
Serikali kuu maboresho haya yalianza na Wizara 5 za Kisekta na upande wa
Serikali za Mitaa mfumo huu ulifanyiwa majaribio kwenye Halmashauri 38 mwaka
1999-2002. Mfumo wa IFMs (Epicor 9.05)
ulioanzishwa unasaidia utunzaji wa kumbukumbu za kihasibu na usimamizi wa fedha
ikiwa ni pamoja na utumiaji wa mfumo katika kutunza hesabu za Halmashauri. Hadi
sasa Mikoa 21 na Halmashauri 133 zimeunganishwa kwenye mfumo huu na mpango wa
Serikali hadi kufikia mwaka wa fedha 2014/2015 ni kuunganisha pia Mikoa na
Halmashauri mpya zote zilizoanzishwa.
Mfumo huu wa usimamizi wa fedha upo ili kudhibiti
upotevu na matumizi mabaya na pia unauhakikishia umma kwamba kuna matumizi
mazuri ya fedha na rasilimali nyingine,
uwajibikaji, uwazi, na kwamba matumizi ya fedha hizo yanaonesha thamani halisi
ya fedha zilizotumika (value for money).
4.2
Vyombo
vingine vya udhibiti
Pamoja na
kuwepo kwa maelezo ya wazi kuhusu wajibu na majukumu ya kila Kiongozi na Mtendaji,
Sheria, Kanuni na Taratibu za usimamizi wa fedha za Mamlaka za Serikali za
Mitaa zimeainisha mfumo na vyombo
vinavyoangalia utekelezaji wa shughuli za Halmashauri zilizopangwa ikiwemo kuhakikisha
miongozo bora ya Uhasibu na utunzaji fedha inazingatiwa. Vyombo hivyo ni pamoja
na:-
a. Mkaguzi
wa Ndani
Halmashauri
zinapaswa kuwa na Mkaguzi wa Ndani kwa mujibu wa Kifungu cha 45 cha Sheria za
Mamlaka za Serikali za Mitaa. Wajibu wake ni kukagua na kutathmini umadhubuti
na ukamilifu wa Mfumo wa Udhibiti wa ndani ambao umewekwa kuhakikisha malengo
ya Taasisi yanafikiwa. Serikali imeendelea kuboresha Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
cha Halmashauri kwa kuwapatia vitendea kazi na mafunzo mbalimbali ili
kuwajengea uwezo katika kuhakikisha udhibiti wa rasilimali za Halmashauri
unaimarika.
b.
Kamati ya Ukaguzi ya Halmashauri
Kamati ina wajumbe wa ndani na nje ya Halmashauri.
Wajibu wake ni kutathmini mpango kazi na taarifa za Mkaguzi wa Ndani, kuhakikisha taarifa za Mapato na Matumizi ni sahihi,
za kuaminika na kamilifu (accurate,
reliable and complete), hivyo kupunguza/kuondoa uwezekano wa kupata hati
chafu za Ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Kadhalika kutoa maoni na ushauri kwa Afisa
Masuuli kuhusu masuala yanayohusu hoja mbalimbali za ukaguzi na udhaifu wa
usimamizi wa fedha ili kurekebisha kasoro zilizobainika na hatimaye kuwezesha rasilimali kutumika kwa
uadilifu na kwa madhumuni yaliyokusudiwa.
c.
Kamati
ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)
Kamati hii ina wajibu wa kupitia taarifa za fedha
zinazowasilishwa na Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali za kila mwaka pamoja na majibu ya hoja hizo;
kuchambua na kuhakiki taarifa za mapato, matumizi na utekelezaji wa miradi ya
maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na kuhakiki miradi ya
maendeleo na matumizi ya mifuko ya pamoja. Katika kutekeleza majukumu hayo,
Kamati hufanya Vikao ambapo Halmashauri hutakiwa kuwasilisha taarifa zao za
mapato na matumizi na kisha kujadiliwa na kupewa maelekezo au mapendekezo ya
namna ya kuboresha utendaji wa kazi. Aidha Kamati pia hutembelea na kukagua
miradi ya maendeleo kulingana na mipango ya Halmashauri ili kuona kama thamani
ya fedha imepatikana na huduma hizo zinakidhi mahitaji ya wananchi.
OWM – TAMISEMI
inaendelea kushirikiana na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za
Mitaa ili kuhakikisha kuwa Sheria, Kanuni na Taratibu za Fedha za Serikali za
Mitaa zinafuatwa na kila mhusika, pamoja na kuona kuwa Halmashauri
zinajirekebisha na kuendelea kupata Hati Safi. Vilevile Ofisi hii pia
imeendelea kuhakikisha kuwa inawachukulia hatua za kinidhamu Watendaji ambao
siyo waadilifu katika masuala ya fedha kwa mujibu wa Sheria.
d.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mujibu wa Kifungu namba
48 cha Sheria ya Fedha ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa amepewa Mamlaka ya
kukagua rasilimali, mifumo ya uendeshaji, utekelezaji wa shughuli za Miradi ya
Maendeleo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, na kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi
namba 19/2008 anapaswa kukagua na kutoa taarifa yenye hati za maoni kuhusu
taarifa za fedha jinsi zinavyoonesha utekelezaji wa shughuli za Mamlaka za
Serikali za Mitaa kila mwaka pamoja na Kufanya ukaguzi maalum pale inapobidi.
Kiuhalisia Halmashauri zimeendelea kufunga vitabu
na kuwasilisha hesabu hizo kwa Wakaguzi kwa wakati. Kwa mujibu wa taarifa ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, hali ya usimamizi na utunzaji
wa vitabu vya hesabu za fedha kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa imeendelea
kuimarika. Mtiririko wa Hati kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa unaonesha kuwa
hati zisizoridhisha zimeendelea kupungua, mfano mwaka 2011/12 hakuna Halmashauri
iliyopata Hati isiyoridhisha ikilinganishwa na Halmashauri nne za mwaka 2005/06.
Kadhalika kwa miaka nane iliyopita hati safi zimeendelea kuongezeka ambapo
mwaka 2011/12 Halmashauri 104 sawa na asilimia 78 zilipata Hati Safi ikiwa ni
ongezeko la Halmashauri 51 kutoka Halmashauri 53 za mwaka 2005/06.
Mwenendo
wa matokeo ya Ukaguzi wa Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa miaka nane
(8) ni kama inavyoonekana katika jedwali linalofuata.
|
Mwaka
|
Hati Safi
|
Asilimia
|
Hati Yenye
shaka
|
Asilimia
|
Hati Chafu
|
Asilimia
|
Hakuna maoni (Disclaimer
|
Asilimia
|
Jumla
|
|
2004/5
|
62
|
53%
|
51
|
44%
|
4
|
3%
|
-
|
-
|
117
|
|
2005/6
|
53
|
43%
|
67
|
54%
|
4
|
3%
|
-
|
-
|
124
|
|
2006/7
|
100
|
81%
|
24
|
19%
|
-
|
-
|
-
|
-
|
124
|
|
2007/8
|
72
|
54%
|
61
|
46%
|
-
|
-
|
-
|
-
|
133
|
|
2008/9
|
77
|
58%
|
55
|
41%
|
1
|
1%
|
-
|
-
|
133
|
|
2009/10
|
66
|
49%
|
64
|
48%
|
4
|
3%
|
-
|
-
|
134
|
|
2010/11
|
72
|
54%
|
56
|
42%
|
5
|
4%
|
-
|
-
|
133
|
|
2011/12
|
104
|
78%
|
29
|
21%
|
-
|
-
|
1
|
1
|
134
|
Ni
mategemeo ya Serikali kuwa Halmashauri nyingi zaidi zitaendelea kupata hati
safi kutokana na jitihada mbalimbali za udhibiti na usimamizi wa fedha
zinazoendelea ikiwemo matumizi ya mfumo wa IFMS-Epicor 9.05, pamoja na
uimarishwaji wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Halmashauri pamoja na Ofisi za
Mikoa zinazosimamia utekelezaji wa shughuli za Halmashauri kwa karibu zaidi.
HATUA ZA KINIDHAMU ZILIZOCHUKULIWA KWA WATENDAJI
Pamoja na kuimarika kwa usimamizi wa rasilimali za MSM,
kumekuwepo na vitendo vya baadhi ya Watendaji katika ngazi hizo kufuja mali za
umma kinyume na taratibu zilizopo. Hata hivyo Serikali imeendelea kuwachukulia Watumishi
hao hatua za Kinidhamu na Kisheria kulingana na makosa waliyofanya. Hatua hizi
ni pamoja na kufukuzwa kazi, kupewa onyo, kuvuliwa madaraka, kushushwa
mshahara, kufikishwa Mahakamani pamoja na kutakiwa kurejesha fedha zilizopotea.
Hatua hizo zimekuwa zikichukuliwa pale inapobainika au kuthibitika Watumishi
wameshindwa kutekeleza wajibu wao. Hadi kufikia mwezi Septemba, 2013 hatua za
Kinidhamu/Kisheria zimechukuliwa kwa Watumishi mbalimbali waliofanya ubadhirifu
kama inavyoonesha katika mchanganuo hapa chini:-
Jumla ya Wakurugenzi 53, Wakuu wa Idara 65 na Watumishi
wengine 749 katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wamechukuliwa hatua mbalimbali
za kinidhamu kufuatia kuhusishwa na ubadhirifu wa fedha za umma kama
ifuatavyo:-
1.
Wakurugenzi;
(i)
Waliofukuzwa Kazi ni
mmoja (1),
(ii)
Waliosimamishwa kazi
ni sita (6),
(iii)
Waliovuliwa Madaraka
ni ishirini na tano (25),
(iv)
Waliopewa ONYO ni kumi
na mbili (12),
(v)
Waliofikishwa Mahakamani
ni nane (8) na
(vi)
Walioshushwa mshahara
ni mmoja (1).
2.
Wakuu wa Idara;
(i)
Waliofukuzwa kazi ni
14,
(ii)
Waliosimamishwa kazi
ni 12,
(iii)
Waliopewa ONYO ni 16,
(iv)
Waliovuliwa madaraka
ni tisa (9),
(v)
Waliofikishwa Mahakamani
ni 13 na
(vi)
Waliofikishwa Polisi
na TAKUKURU ni mmoja (1).
3.
Watumishi wengine;
(i)
Waliofukuzwa kazi ni
217,
(ii)
Waliosimamishwa kazi
ni 168,
(iii)
Walioshushwa cheo ni
wanne (4),
(iv)
Walioshushwa cheo ni
28,
(v)
Waliopewa ONYO ni 85,
(vi)
Waliofikishwa Mahakamani
ni 212 na
(vii)
Waliofikishwa Polisi
na TAKUKURU ni 35.
CHANGAMOTO ZINAZOZIKABILI MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA
Pamoja
na jitihada za Serikali za kuhakikisha MSM zinawezeshwa ili kutoa huduma bora
kwa wananchi bado, zipo changamoto mbalimbali ambazo zinaendelea kupatiwa
ufumbuzi. Miongoni mwao ni pamoja na:-
1.
Utegemezi mkubwa wa fedha
za Ruzuku kutoka Serikali Kuu ili kutekeleza shughuli za maendeleo. Mapato ya
ndani ya Halmashauri yanayokusanywa hayatoshi kukidhi mahitaji ya wananchi
hivyo kuzifanya Mamlaka za
Serikali za Mitaa kutegemea Ruzuku na Misaada ya Washiriki
wa Maendeleo. Hata hivyo, Halmashauri zimeendelea kuhimizwa kubuni vyanzo vipya
vya mapato na kuhakikisha vile vilivyopo vinakusanywa kwa ukamilifu.
2.
Baadhi ya watumishi
kutokuwa waaminifu na kuendelea kutumia fedha za umma isivyo halali.
3.
Uhaba wa watumishi na
vitendea kazi.
4.
Baadhi ya wadau mbalimbali
kutokukubali Mfumo wa usimamizi wa fedha ulioanzishwa wa IFMS – Epicor 9.05.
MIKAKATI ILIYOWEKWA KUONGEZA UWAJIBIKAJI NA NIDHAMU
KATIKA MATUMIZI NA KUDHIBITI UBADHIRIFU WA MALI/FEDHA ZA UMMA
Mikakati
iliyowekwa na Serikali ili kuongeza uwajibikaji na udhibiti wa mali za Umma ni
kama ifuatavyo:-
1.
Kutoa maelekezo kwa
Halmashauri zote nchini kufanya ukaguzi wa mara kwa mara hususan katika miradi
ya maendeleo kwa kutumia vyombo vifuatavyo:-
a.
Timu ya Menejimenti ya Halmashauri (CMT),
b.
Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango,
c.
Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani,
d.
Kamati ya Ukaguzi ya Halmashauri, na
e.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
2.
Kuendelea kuzijengea
uwezo Sekretarieti za Mikoa ili ziweze kushauri na kusimamia utekelezaji wa shughuli
za Halmashauri ikiwemo ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kuchukua hatua stahiki
wa watumishi watakaobainika kufanya ubadhirifu.
3.
Kuendelea kuimarisha Kitengo
cha Ukaguzi wa Awali na Kitengo cha
Ukaguzi wa Ndani wa Halmashauri kwa kuwapatia Wakaguzi wa ndani vitendea kazi
ili kurahisisha ufuatiliaji katika maeneo yao, sambamba na kuendelea kufanya
mafunzo kwa Wakaguzi wote wa Ndani wa
Halmashauri na wale walio Mkoani.
4.
Viongozi wa
OWM-TAMISEMI pamoja na Wataalam kuendelea kufuatilia na kufanya ukaguzi kwa
Mikoa na Halmashauri kwa lengo la kuangalia uendeshaji wa shughuli za
Halmashauri ikiwa ni pamoja na Miradi ya Maendeleo. Pia
kupeleka nyenzo kama magari, pikipiki na Kompyuta.
5.
Kuendelea kuimarisha
mifumo ya uhasibu na udhibiti wa ndani
kupitia Mfumo wa usimamizi wa fedha wa IFMS- EPICOR 9.05 kwa upande wa “technical“ na “application“ ili kuhakikisha nidhamu ya bajeti na taratibu za
matumizi ya fedha vinafuatwa. Hii itahusisha marekebisho katika Mtandao wa
mawasiliano hususan Halmashauri za pembezoni pamoja na kukamilisha “module” mbalimbali zitakazotumika katika
uaandaji wa taarifa za fedha na ufungaji wa Hesabu. Mfumo pia utaendelea
kutumika kufuatilia kwa karibu na kudhibiti matumizi yanayofanywa na
Halmashauri moja kwa moja kulingana na Sheria za Fedha.
6.
Kufunga Mfumo wa
IFMS-EPICOR 9.05 katika Halmashauri na Mikoa mipya iliyoanzishwa pamoja na
kutoa mafunzo kwa Waweka Hazina na Wahasibu wa Halmashauri JUU ya namna ya
kuutumia ipasavyo.
7.
Kuendelea kutoa miongozo
mbalimbali kwa Mikoa na Halmashauri juu ya matumizi sahihi ya fedha za Umma
pamoja na kuendelea kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wanaobainika
kufanya ubadhirifu wa mali ya Umma kulingana na Sheria zilizopo.
8.
Kuendelea kutoa mafunzo
kwa watendaji wa Halmashauri na Mikoa juu ya usimamizi wa fedha, manunuzi,
ukaguzi na majukumu yao kwa wananchi pamoja na uwajibikaji.Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.



0 comments:
Post a Comment