Home » » Gharama kubwa ya umeme yatishia kuwakimbiza wateja

Gharama kubwa ya umeme yatishia kuwakimbiza wateja

Shirika la Umeme nchini (Tanesco)
 
Wananchi  wakereketwa wametishia kugomeea kutumia umeme wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), kama shirika hilo halitapunguza bei ya nishati hiyo.
Wakereketwa hao ambao walijitokeza jijini Dar es Salaam na kuzungumza na waandishi wa habari walidai kuwa Tanesco inatakiwa kupunguza kiwango hicho cha umeme kabla ya Februari 21, mwaka huu.

Walisema kama baada ya tarehe hiyo Tanesco itakuwa bado haijashusha bei ya umeme, hawatakuwa tayari kuitumia nishati hiyo.

Walisema mpaka Februari 21, mwaka huu, siku hizo zinatosha kwa shirika hilo kukaa na kuangalia uwezekano wa kupunguza bei ya umeme.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, kiongozi wa wananchi hao, Sheikh Rashid Kayumbo, alisema kupanda kwa bei ya umeme kumechangia kuongezeka kwa gharama ya maisha.

Aidha, alisema kupanda kwa nishati hiyo kumechangia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa viwandani na zile za mashambani kupanda bei.

Alitoa mfano kuwa bei ya mfuko wa saruji iliyokuwa ikiuzwa kati ya Sh.13,500 hadi 14,000, sasa inauzwa kati ya Sh. 15,500 na Sh. 16,000.

“Tulidhani kupanda kwa gharama hizi kutachangia kuleta mabadiliko katika ununuzi wa mitambo, kuboresha upatikanaji wa umeme ikiwamo kuondoa mgawo wa umeme, lakini hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika,” alisisitiza Sheikh Kayumbo.

Aliongeza kuwa gharama kubwa za umeme zimekuwa mzigo mkubwa hasa kwa wananchi wa kipato cha chini na nishati hiyo sasa inaoonekana kama anasa badala ya kuwa mahitaji ya lazima kwa kila mtu.
CHANZO: NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa