TANZIA
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inasikitika kutangaza kifo cha Diwani
wa kata ya Mbweni Mh. Boniface Mnyachibwe kilichotokea leo ghafla saa
tatu asubuhi.
Tunatoa pole kwa familia yake, wakazi wa Mbweni, Wananchi wa Kinondoni pamoja na Chama chake cha CCM.
Mchango wake mkubwa ktk kuboresha maisha ya wakazi wa Mbweni na
Kinondoni kwa kujituma na uadilifu kamwe hautasahaulika. Aidha, kifo
chake cha ghafla leo wakati jana tulikuwa naye mpaka saa moja na nusu
jioni kwenye vikao vya bajeti ni uthibitisho wa uzalendo wake na mapenzi
yake kwa anaowawakilisha na Kinondoni kwa ujumla.
Dua zetu na sala zetu ziende kwa familia yake na wote aliokuwa anawawakilisha.
Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahala pema peponi.Imetolewa na Manispaa Ya Kinondoni
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Home »
» DIWANI WA KATA YA MBWENI BONIFACE MNYACHIBE(CCM)AFARIKI DUNIA

0 comments:
Post a Comment