Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC), ina mpango wa kujenga uwezo
wa kuzalisha umeme wake ili kupunguza au kuondoa tatizo la nishati hiyo
wakati wa uzalishaji.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni mwendelezo wa kiwanda
hicho kuboresha mkakati wake wa biashara, kuhakikisha bidhaa ya saruji
inayozalishwa kiwandani hapo inamfikia mteja kwa bei nafuu.
Akizungumza kwenye chakula cha jioni kwa
wasambazaji saruji kutoka maeneo mbalimbali nchini mjini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkurugenzi Mtendaji wa TPCC, Alfonso
Rodriguez alisema kampuni yake imeamua kuweka mfumo mpya wa mkakati
kukabiliana na ushindani wa soko.
Rodriguez alisema kampuni hiyo kila mwaka ina
utaratibu wa huandaa chakula cha jioni kwa wasambazaji wake nchini,
lengo likiwa ni kubadilishana mawazo na uzoefu wa biashara ya saruji
nchini.
Hata hivyo, Rodriguez alipongeza hatua za Serikali
inazochukua kudhibiti uagizaji saruji kwa njia za panya na kuuzwa kwa
bei ya chini, kwani kitendo hicho kinasababisha ushindani usio wa haki.
Akiwasilisha ripoti ya masoko kwa wasambazaji,
Rodriguez alisema Twiga Cement kama ilivyo kwa kampuni nyingine za
saruji imekuwa ikikabiliana na changamoto kubwa kwa soko nchini.
Alisema changamoto hiyo inasababishwa na uagizaji
na udhibiti hafifu wa saruji kutoka nje ya nchi, hususan Pakistan na
tatizo la mgawo wa umeme unaopunguza uzalishaji kwa kiwango kikubwa.
Katika hafla ya mwaka huu kampuni ya Nayan
Enterprises iliinuka kidedea kwa kuwa msambazaji bora wa mwaka nafasi ya
pili ikichukuliwa na Mwanza Huduma Ltd ya tatu ikiwa kampuni ya VGK na
Texas Hardware ikishika nafasi ya nne.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment