Home »
» TUME YAANDAA MKAKATI KUUNGANISHA USHIRIKA, SACCOS
TUME YAANDAA MKAKATI KUUNGANISHA USHIRIKA, SACCOS
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
TUME
ya Maendeleo ya Ushirika imeandaa mkakati kwa kuunganisha vyama vya
ushirika vya uzalishaji na vya akiba na mikopo (SACCOS) ili kuinua
vipato vya ushirika.
Hayo yameelezwa jana na Mrajis wa vyama vya
Ushirika na Mkurugenzi Audax Rutabanzibwa alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Rutabanzibwa alisema
wameamua kufanya hivyo baada ya kuona vyama vingi vya ushirika
vinakwenda kukopa benki na kupewa riba kubwa huku mzigo wa deni hilo
akibebeshwa mwanachama ambaye ni mzalishaji.
"Tumeangalia tukaona
kuna vyama vya akiba vina zaidi ya bilioni 20 benki halafu vinakopeshwa
ukiangalia hizo fedha ni wanachama ambao wanakwenda kukopa tena kwa riba
wakati wanaweza kukopeshana wenyewe na bila riba cha msingi ni
uzalishaji," alisema.
Alisema kuwa zipo baadhi ya benki ambazo riba
zao ni kubwa hivyo hufanya vyama vya ushirika kushindwa kusonga mbele na
kuwawezesha wanachama kuwa na maendeleo kutokana na mikopo.
Alisema
kuwa endapo vya mahivyo vitafanya mchakato huo wanachama wanafaidika na
vyama vyao kwa kurudisha kwa wakati na kwa riba ndogo na kupata
maendeleo.
Rutabanzibwa aliendelea kueleza mazungumzo yameanza kati
ya Tanga Diary Corporative na Posta na Simu Saccos LTD na yanaendelea
vizuri ambapo kufikia mwezi wa tatu makubaliano yatakuwa yamefikiwa.
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment