Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Seleman Rashid.
Hatua hiyo inakuja kufuatia kuibuka wimbi la matukio ya madaktari feki katika hospitali za serikali.
Aidha, amesema watu wote waliopewa mamlaka ambao wanashindwa kuwajibika ipasavyo na kusababisha madaktari feki kujipenyeza katika hospitali hizo na kuanza kutoa huduma za afya uchunguzi wa kina utafanyika kuwabaini na watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aliyasema hayo jana wakati akizungumza katika mahojiano na kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Radio One.
Kipindi hicho kilikuwa kikijadili hatua gani madhubuti zinachukuliwa na wizara kukomesha tatizo madaktari feki katika hospitali za serilali.
“Tunalaani kitendo cha mtu kuingia na kufanya kazi ya udaktari wakati siyo daktari katika eneo la tiba ambalo ni la kitaalam, pili wale wote ambao wameshiriki kusababisha kitu hiki kutokea kuanzia walinzi, uongozi na mkuu wa idara ambao wamempokea huyo mtu watatdibitiwa na hatua kali zitachukuliwa,” alisema.
Alisema kutokana na mfululizo wa matukio hayo, serikali imejipanga kuanzisha mfumo wa kielektroniki katika maeneo ya wizara na vyuo vyote vya afya vinavyozalisha wataalam wa afya.
Alifafanua kuwa katika vyuo hivyo kutakuwa na mfumo huo ambao utakuwa unamtambua mtu kama ni mfanyakazi au siyo kwa kutumia alama za vidole ambao utaeleza mhusika amejiriwa lini na amepangiwa kufanya kazi gani.
Aidha, alisema katika tukio lililotokea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), ameiachia Bodi ya hospitali hiyo kufanya uchunguzi na kuchukua hatua ambapo yeye atapewa taarifa.
Tamko la waziri likekuja siku mbili tu baada ya kukamatwa kwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Kitano Mustafa Kitano,katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambaye inadaiwa amekuwa akiendesha shughuli za kitapeli hospitalini hapo kwa muda mrefu huku akijidai kuwa ni daktari wa uzazi.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment