Home » » TMA YATAHATHARISHA HALMASHAURI MVUA ZAA MASIKA

TMA YATAHATHARISHA HALMASHAURI MVUA ZAA MASIKA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi.
 
Mamlaka  ya Hali ya Hewa (TMA)  imezitaka halmashauri za miji kuchukua tahadhari pamoja na kusafisha miundombinu ya maji taka na mitaro ili kupunguza athari za maji kutuama na kutokea mafuriko katika kipindi cha mvua za masika zitakazoanza Machi hadi Mei mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  jana, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi alisema viashiria vinavyosababisha mvua za masika mwaka huu ni kuwapo kwa joto la chini  la wastani katika eneo la Bahari ya Atlantiki (Pwani ya Angola) ambalo linatarajiwa kuwapo kwa kipindi chote cha msimu.

Alisema mvua za masika  zitanyesha katika maeneo ya Kaskazini mwa nchi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka na zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza ya mwezi Machi.

Alisema mvua hizo zinatarajiwa kuanza Kanda ya Ziwa Victoria katika mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Shinyanga na Simiyu na zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza kwenye mikoa ya Geita na Kagera na kusambaa mikoa mingine katika wiki ya pili na inatarajiwa kupata mvua za juu ya wastani.

Aidha, alisema katika Nyanda za Juu Kusini Magharibi yenye mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa na Katavi, mvua zinazoendelea kunyesha zinatarajia kuwa za wastani hadi juu ya wastani isipokuwa maeneo ya mikoa ya Njombe ambapo zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani.

Alisema maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za juu ya  wastani kuna uwezekano wa milipuko ya magonjwa kama vile malaria, kipindupindu, kuhara damu na homa za matumbo.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa