Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waandishi wa Habari wa Kampuni ya Mwananchi Communications
Limited (MCL) inayochapisha magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti na The
Citizen wanaongoza katika orodha ya wateule wa Tuzo za Umahiri wa
Uandishi wa Habari 2013 (Ejat 2013) kwa kuingiza majina 15 kati ya 76 ya
wateule watakaotunukiwa zawadi zao Machi 14 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa hafla ya kutaja majina ya
wateule hao, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Taifa la Habari
(MCT), Pili Mtambalike alisema mchujo huo umefanywa na jopo la majaji
lililoongozwa na mkufunzi na mhariri wa habari wa siku nyingi nchini,
Gervas Moshiro.
Mtambalike alisema washindi watatunukiwa tuzo zao
na Rais wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jaji Harold Nsekela
katika hafla itakayofanyika Machi 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Jumla ya kazi 907 ziliwasilishwa kwa ajili ya kuwania tuzo hizo.
Alisema majaji walizipitia na kupitisha kazi 101
ambazo ni pamoja na za magazeti (46), redio (39) na televisheni (16) na
kulingana na takwimu hizo, idadi ya kazi za redio imeongezeka kutoka 21
za mwaka 2012 na magazeti kazi tano zaidi zimeongezeka.
Kazi za televisheni zimepungua kwa idadi ya tatu
kutoka 19 za mwaka 2012. Idadi ya kazi zilizopitishwa katika mchujo wa
majaji hao zimeongezeka kutoka 76 hadi 81, kiwango ambacho ni sawa na
ongezeko la asilimia 24.6.
Mtambalike alisema pia idadi ya washiriki wanawake
nayo imeongezeka kutoka washiriki 12 hadi 18 kwa mwaka 2013, ongezeko
ambalo ni sawa na asilimia 63.6. Alisema ili majaji kuwapata wateule hao
walilazimika kufanya kazi ya ziada kutokana na ushindani uliokuwepo.
Kwa upande mwingine, kaimu mkurugenzi huyo
alisema, jopo la wataalamu chini ya uenyekiti wa mhariri wa siku nyingi
na mtalaamu wa masuala ya habari, Theophil Makunga, bado lipo katika
mchakato wa uteuzi wa jina linalostahili kushinda Tuzo ya Maisha ya
Mafanikio na Uandishi wa Habari (LAJA).
Waandishi wa Magazeti ya Mwananchi na The Citizen
ambao majina yao yametajwa katika wateule wa tuzo hizo kwa mwaka 2013 ni
pamoja na Fred Azzah, Florence Majani, Polycarp Machira, Kalunde Jamal,
Herieth Makweta, Beldina Nyakeke, Sheilah Sezzy, Elias Msuya,
Jacqueline Masinde na Athuman Mtulya.
Wengine ni Fidelis Felix, Kelvin Matandiko,
Phinias Bashaya, Zephania Ubwani, Mussa Juma.Waandishi hao wa MCL
wameongezeka kwa idadi ya mwandishi mmoja ikilinganishwa na idadi ya
wateule 14 wa tuzo zilizopita.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment