Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) imesema itatoa mamlaka kamati
yake ya Ufundi kuteua wachezaji watakaoiwakilisha nchi kwenye Michezo ya
Jumuiya ya Madola endapo vyama vya michezo vitashindwa kuwateua
wachezaji wao wenye viwango hadi Jumamosi hii.
Tanzania itawakilishwa na timu za judo, ngumi,
riadha, kuogelea, mpira wa meza, paralimpiki, baiskeli na kunyanyua vitu
vizito kwenye michezo hiyo iliyopangwa kufanyika katikati ya mwaka
nchini Scotland.
Akizungumza na Gazeti hili makao makuu ya kamati
hiyo jijini jana, Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi alisema endapo vyama
vitashindwa kuthibitisha idadi ya wachezaji wake kamati yao ya ufundi
Jumamosi hii itachukua jukumu hilo.
“Awali vyama vilituletea majina mengi ya wachezaji
tukawaambia waende na walete majina ya wale tu wenye viwango vya
kushiriki madola na mwisho ilikuwa ni leo ‘jana’ lakini hadi sasa hivi ‘
jana saa tano asubuhi’ hakuna hata chama kimoja kilichofanya hivyo,”
alisema Bayi.
Alisema endapo vyama hivyo vitashindwa kupeleka majina
hayo Kamati ya Ufundi ya TOC itakayokutana Jumamosi itachukua jukumu
hilo
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment