Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Bingwa wa zamani ya ngumi wa Jumuiya ya Madola kwenye uzani wa
Bantam, Michael Yombayomba amemwomba Rais Jakaya Kikwete amrudishe
kazini.
Yombayomba bondia pekee aliyewahi kuiletea
Tanzania medali ya dhahabu ya Jumuiya ya Madola aliyasema hayo hivi
karibuni katika mahojiano na gazeti hili nyumbani kwao Kibaha.
“Ninachokiomba hivi sasa ni huruma ya Rais Kikwete
ili nirudishwe kazini, maisha ‘yamenipiga’ na kazi ndiyo kila kitu
kwangu, hivi sasa naadhirika,” alisema Yombayomba.
Bondia huyo ambaye pia aliwahi kutwaa medali ya
shaba ya michezo ya Afrika alisema amekuwa akiishi maisha magumu ya
dhiki baada ya kufukuzwa kazi mwaka 2002 hadi leo na kufikia hatua ya
kufanya vibarua vya hapa na pale ili kujikimu.
“Niliongea na Rais siku ya sherehe ya Kifimbo cha
Malkia kwenye Viwanja vya Ikulu na kumweleza matatizo yangu, najua ana
majukumu mengi, lakini kupitia gazeti la Mwananchi naomba anisaidie
nirudishwe kazini,” alisema Yombayomba.
Bondia huyo alifukuzwa kazi miaka michache baada
ya kupewa usajenti kutokana na kushinda medali ya dhahabu ya Jumuiya ya
Madola, hata hivyo alifukuzwa ndani ya saa 24 kwa kile alichoeleza ni
kuondoka kwenye kambi ya timu ya taifa na kwenda kuiaga familia yake
kabla ya safari ya Uingereza kwenye michezo ya Madola ya msimu huo na
kudaiwa kutoroka kambini hivyo kufunguliwa kesi ya utoro jeshini.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment