Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KAMPUNI ya LG, imezindua friji mpya ambayo ina uwezo wa kuendelea kufanyakazi kwa masaa 10 baada ya umeme kukatika.
Akizungumza Dar es
Salaam jana, meneja wa bidhaa za LG Tanzania Mayur Parikh, alisema kuwa
friji hiyo ina uwezo mkubwa wa kufanya kazi baada ya umeme kukatika
ambapo ina uwezo wa kugandisha kwa muda wa masaa 10 bila umeme.
Alisema kuwa wameamua
kuizindua bidhaa hiyo mahususi kutokana na matatizo ya kukatika kwa
umeme mara kwa mara ambayo hutokea katika maeneo mbalimbali nchini.
Alisema kuwa tatizo la
kukatika kwa umeme mara kwa mara, limepelekea kampuni yao kutanua wigo
wa matumizi ya bidhaa zao na kuamua kuzindua friji hiyo.
Alisema kuwa teknolojia
waliyoitumia katika utengenezaji wa bidhaa hiyo ni ya aina yake ambapo
baada ya umeme kukatika friji itaendelea kufanya kazi kwa kutumia mfumo
maalumu uliotengenezwa kitaalam.
Alisema kuwa pia friji hiyo inatumia umeme mdogo tofauti na zilivyo zingine, ambapo mteja anaweza kuitumia katika eneo lolote.
“Tumeamua kuzindua
bidhaa hii mpya kwa ajili ya kutoa fursa wa watumiaji kutopata shida
katika kipindi umeme unapokatika kwani kuna sehemu ambayo inaweza
kuendelea kuhifadhi vyakula kwa muda wa masaa 7 na nyingine masaa 10
bila kuharibika,” alisema.
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment