Home » » Kampuni D’salaam yaanza kukopesha matrekta wakulima

Kampuni D’salaam yaanza kukopesha matrekta wakulima

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Kampuni ya Intertechnology Ltd ya Dar es Salaam, imeanza kuuza na kukopesha matrekta yenye gharama nafuu kwa wakulima kwa lengo la kuongeza kasi ya mapinduzi ya kijani katika sekta ya kilimo.
Mbali na hayo, pia kampuni hiyo imesema inatekeleza sera ya kilimo kwanza kwa kuhakikisha kila mwananchi anapata uhakika wa kuongeza kipato kupitia kilimo.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Dk. Francis Mayaka wakati akizindua matrekta hayo yaliyotengenezwa nchini Belarus yenye ukubwa wa injini HP40 mpaka 320.
Dk. Mayaka alisema kuwa kila trekta litauzwa kuanzia kiasi cha Sh30 milioni hadi Sh35 milioni ili kuwafikia Watanzania wengi kwa lengo la kuhakikisha kila mmoja anakuza uchumi kupitia sekta ya kilimo.
“Tumelenga kila mkulima nchini apate fursa ya kununua trekta la kisasa kwa bei nafuu kuanzisha ukubwa wa injini HP40 hadi HP320 tofauti na baadhi ya matrekta mengi yaliyopo nchini sasa yenye uwezo wa injini kuanzia HP40 hadi HP60.” alisema
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa