Home » » ‘Machinga Mbagala ondokeni barabarani’

‘Machinga Mbagala ondokeni barabarani’

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WAFANYABIASHARA wanaofanya shughuli zao pembezoni mwa Barabara ya Kilwa eneo la Mbagala, wametakiwa kuondoka katika maeneo hayo, kutokana na kuwa hayaruhusiwi kufanyia biashara.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Meya wa Manispaa ya Temeke, Mabadi Hoja wakati akizungumza na gazeti hili kuhusiana na wafanyabiashara hao, ambao wamekuwa wakifanya biashara pembezoni mwa barabara.
Alisema kitendo cha kufanya biashara pembeni mwa barabara hiyo, kinahatarisha maisha yao na ya wateja wao.
Hoja alisema tayari amri ilishatolewa kuwa wafanyabiashara wote, wanaofanya shughuli zao katika maeneo yasiyoruhusiwa, waondoke, lakini wamekaidi agizo hilo hivyo wanajipanga kuwachukulia hatua zaidi.
"Wale wanatakiwa waondoke, hawaruhusiwi kufanya biashara katika maeneo hayo, lakini wamekaidi tu, si unajua tena sisi Watanzania tulivyo wabishi. Lakini tumeshangawatangazia waondoke," alisema Hoja.
Aliongeza kuwa kwa sasa suala hilo wanalifanyia kazi, pia imeundwa kamati maalumu ya kufuatilia suala hilo, kwani si la kukurupuka mara moja.
"Hata Mkuu wa Mkoa alishatangaza kuwa anayefanya biashara katika maeneo yasiyohusika, aondoke. Kwa hiyo hili suala huwezi tu ukaanza kuwapiga watu na kuwataka waondoke, wataondoka tu," aliongeza.
Chanzo;Habari Leo

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa