Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » MANISPAA YA KINONDONI MNALIONA HILI: WAFANYABIASHARA WANAFANYA KAZI CHINI YA NYAYA ZA UMEME MKUBWA WA UBUNGO (SONGAS)‏

MANISPAA YA KINONDONI MNALIONA HILI: WAFANYABIASHARA WANAFANYA KAZI CHINI YA NYAYA ZA UMEME MKUBWA WA UBUNGO (SONGAS)‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Hapa ndipo makao Sogas yaliyopo Ubungo kwenye wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Sehemu hii inatumika kuzalisha umeme unaotumika kwenye grid ya Taifa. Lakini kuna wafanyabiashara wanaofanyia kazi zao nje ya jengo hilo la kuzalishia umeme na limeonekana kama limepotezewa na kuona kama ni kitu cha kawaida sana.
Unaweza kusema watu wanaigiza lakini huu ndio ukweli maana watu wanfanya biashara katika eneo ambalo ni hatarishi. Hapo juu yao kuna nyaya kubwa ambazo zinatumika kusambaza umeme unaozaliswa eneo hili na uongozi umelichukulia suala kama ni la kawaida maana hapo Songas kuna walinzi lakini unaweza kujiuliza ni kwa nini wananchi hawa wanafanya biashara kwenye maeneo hatarishi kwa maisha yao
Tazama hapa biashara inaendelea kama kawaida na hakuna anayeliona hili tatizo tunasubiri yakishatokea majanga ndio tutaanza kuwaondoa wafanya biashara hao.

PICHA NA PAMOJA BLOG

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa