Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WASHITAKIWA 11
katika kesi ya kuporomoka jengo la ghorofa 16 kwenye mtaa wa Indira
Gandhi, Dar es Salaam, wamepelekwa rumande baada ya kubadilishiwa hati
ya mashitaka.
Pamoja na
mmiliki wa jengo hilo, Raza Ladha (68), waliokuwa nje kwa dhamana
wakikabiliwa na mashitaka ya kuua bila kukusudia watu 24 katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, jana walibadilishiwa mashitaka na kuwa ya kuua
kwa kukusudia.
Katika kesi hiyo, aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime ameongezwa.
Wengine ni
mhandisi wa jengo hilo, Goodluck Mmbanga (35), Mkaguzi wa jengo Willbrod
Mugyabuso (42) na Diwani wa kata ya Goba, Ibrahim Kissoky (59), ambaye
ni mfanyabiashara, anayemiliki kampuni ya Lucky Construction ya Dar es
Salaam iliyojenga jengo hilo.
Wamo pia
Mhandisi Mohamed Abdulkarim (61), Mhandisi wa Manispaa ya Ilala Charles
Ogare (48), Mhandisi Mshauri Zonazea Oushoudada (60), anayemiliki
Kampuni ya Sou Consultancy Co. Ltd, ambayo ilikuwa ikisimamia ujenzi wa
jengo hilo, Msanifu Majengo Vedasto Nzikoruhale (59) na Mwandaaji
Michoro ya Majengo Michael Hema (59).
Msajili
Msaidizi wa Bodi ya Wasanifu na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Albert Mnuo
(56) na Ofisa Mtekelezaji Mkuu wa AQRB, Joseph Ringo (43).
Walibadilishiwa
mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka na kusomewa 27 ya kuwaua
kwa makusudi watu 27. Hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama
hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.
Wakili wa
Serikali Mkuu Bernard Kongola, aliiomba mahakama kubadilisha hati ya
mashitaka na kumuongeza Fuime na mashitaka kutoka kuua bila kukusudia na
kuwa kuuwa kwa kukusudia.
Fuime aliyekuwa
akikabiliwa na kesi ya kuua watu wanne kutokana na kuporomoka kwa jengo
hilo, Machi 29, mwaka jana, asubuhi alifutiwa mashitaka mbele ya Hakimu
Mkazi Augustina Mmbando.
Hatua hiyo ilitokana na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na mashitaka dhidi yake.
Baadhi ya washitakiwa walionekana kupigwa butwaa waliposomewa mashitaka mapya. Kesi itatajwa Machi 26, mwaka huu.
Chanzo;Uhuru
0 comments:
Post a Comment