Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wiki iliyopita gazeti hili liliandika kwamba fedha hizo
zilitolewa baada ya Serikali kuamua kumaliza shauri hilo na hapo ndipo
fedha hizo zilipochukuliwa katika akaunti hiyo na PAP.
Hata hivyo, pamoja na Seth kukubali kuchukua fedha
hizo, alisema fedha zilizokuwamo ni Sh150 bilioni, huku akitetea hatua
hiyo na ununuzi wa IPTL kwamba siyo kinyume cha sheria.
Kabla ya kuuzwa kwa PAP, IPTL ilikuwa inamilikiwa
kwa ubia kati ya Mechmar Corporation ya Malaysia (asilimia 70) na VIP
Engineering and Marketing Company Limited ya Tanzania iliyokuwa na
asilimia 30.
PAP ni kampuni ya tatu katika mgogoro huo
kujitokeza na kutoa ufafanuzi tangu habari zake zilipoanza kuandikwa.
Kampuni ya kwanza ilikuwa ni VIP Engineering ya James Rugemalira na
baadaye akaibuka Mwanasheria wa IPTL na wote walitetea mauzo hayo.
PAP ilivyonunua IPTL
Wakili wa PAP, Joseph Mwakandege alisema, kwa
miaka mitano ya ITPL iliendeshwa bila kuwapo kwa mgogoro, lakini baadaye
iliibuka mivutano miongoni mwa wanahisailiyosababisha kufunguliwa kwa
akaunti ya Escrow.
Mwakandege alisema 2010, Sethi aliwasilisha
nyaraka mahakamani kuonyesha kwamba alipewa mamlaka ya kusimamia mali
zote za Mechmar hapa nchini.
Alisema, baadaye Sethi alinunua hisa zote ambazo awali Mechmar alikuwa ameuza kwa Piperlink na kuzihamishia PAP.
Kwa mujibu wa wakili huyo, Sethi baadaye alinunua
asilimia 30 zilizosalia, na tayari mmiliki wa VIP, Rugemalira
amekwishakiri kupokea Dola za Marekani 75 milioni (Sh120 bilioni)
alizoziita kuwa ni fedha za ugoro.
Alisema baada ya mauzo hayo, VIP ilikwenda mahakamani na kuomba kesi zote zinazohusu kampuni hiyo na Mechmar zifutwe.
Septemba 5, mwaka jana, mahakama iliamua kufuta
kesi hizo, hivyo PAP akapata haki ya kumiliki mali zote za IPTL, ikiwa
ni pamoja na fedha zilizokuwa katika akaunti ya Escrow.
Mwakandege alisema baada ya uamuzi huo, PAP
ilikubali kulipa madeni yote ya IPTL na ufilisi wa muda uliokuwa
umewekwa kwa kampuni hiyo uliondolewa.
“Kutokana na hali hiyo, ilibidi kusainiwa mkataba kati ya IPTL
na Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini…Ifahamike kwamba akaunti
ya Escrow ilikuwa mali ya wanahisa wa IPTL, haikuwa na fedha za
walipakodi wala fedha za Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong
(mkopeshaji wa IPTL),” alisema Mwakandege.
Alifafanua kuwa, Serikali iliitaka PAP kusaini
makubaliano kwamba iwapo watatokea wadai wapya wa IPTL itawalipa.
Alisema baada ya hapo Serikali iliandika barua kwa BoT kuitaka iruhusu
fedha hizo zilipwe kwa PAP.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment