Mratibu wa mafunzo SACP Patrick Byatao, akitoa mada kwa Mainspekta washiriki katika mafunzo ya kujenga maadili mjini Dodoma.
CP Mussa Ali Mussa, akitoa mada ya utekelezaji wa miradi ya utekelezaji wa miradi ya Polisi Jamii wakati wa mafunzo ya Maadili kwa Mainspekta wa Polisi ambao ni Wakuu wa Majimbo n Tarafa.
Mainspekta wanaoshiriki katika mafunzo ya maadili na rushwa wakiimba wimbo wa maadili kabla ya kuanza kwa mafunzo hao mjini Dodoma.
Mainspekta wa Polisi ambao ni Wakuu wa Mmajimbo na Tarafa wanaoshiriki katika mafunzo ya maadili mjini Dodoma wakimsikiliza Kamishna Mussa Ali Mussa, akitoa mada ya Utekelezaji wa Miradi ya Polisi jamii.
picha ya pamoja na CP Mussa Ali Mussa, katikati waliokaa pamoja na baadhi ya Mainspekta wa Polisi ambao ni washiriki wa mafunzo ya maadili mjini Dodoma.
****
****
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi-Dodoma
Jeshi
la Polisi nchini limebuni mikakati itakayosaidia kukomesha ajali za
barabarani kwa kuvishirikisha vikosikazi vya Polisi Jamii
vilivyotawanywa katika kila kata na tarafa nchini kote.
Mikakati
hiyo imetangazwa na Kamishna wa Polisi Jamii CP Mussa Ali Mussa, wakati
wa mafunzo ya maadili awamu ya pili yanayotolewa kwa Askari Polisi wa
ngazi ya kati yanayoendelea Mjini Dodoma.
Kamishna
Mussa amesema kuwa mpango huo utasaidia kuwanasa madereva wazembe
wasiozingatia taratibu na sheria za usalama barabarani na hivyo
kupunguza ajali ziletazo vifo na majeruhi kwa abiria na watumiaji
wengine wa barabara wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
Amesema
vikosikazi hivyo vinaundwa na askari Polisi kutoka katika vitengo
tofauti na kikubwa vikizingatia kazi ya msingi ya Jeshi la Polisi ya
kuzuia na kukamata makosa mblimbali yakiwemo ya usalama barabarani.
“Kulinda
usalama wa wananchi na mali zao ndiyo kazi kubwa ya Jeshi la Polisi na
kwamba kwa yeyote atakayepatikana akienda kinyume na taratibu za usalama
barabarani atatiwa mbaroni na hakutakua na huruma kwa mkosaji”. Alisema
Kamishna Mussa na kuvitaka pia vikosikazi hivyo kufanya kazi kwa
kuzingatia maadili ya Afisa wa Polisi.
Kwa
upande wake, Kamishna Msaidizi wa Polisi kutoka Kamisheni ya
Intelijensia nchini, ACP Andrew Mwang’onda, alisema kamisheni hiyo
imepanga kuwatumia Mainspekta wakiwemo Wakuu wa Polisi wa Tarafa na
Majimbo hapa nchini katika ukusanyaji wa taarifa za kiintelijensia kwa
lengo la kubaini viashilia vya kihalifu na wahalifu.
Naye
Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Andrew Makungu, ambaye amekokotoa idadi
ya Watanzania, vitongoji, vijiji, kata, shehia, tarafa, majimbo, wilaya
na mikoa iliyopo hapa nchini ikiwemo ya kipolisi, amewataka Mainspekta
hao kuhakikisha kuwa wanashirikiana kwa karibu na wananchi katika
kuwabaini wahalifu na maficho yao ili wakamatwe na kufikishwa
mahakamani.
Awali
Mkuu wa Tathmini na Ufuatiliaji wa Jeshi la Polisi nchini Naibu
Kamishna Mpinga Gyumi, alisema Jeshi hilo limejipanga kuboresha mifumo
ya utoaji huduma bora kwa wananchi na kujenga maadili mema ili kuepukana
na vitendo vya kudai na kupokea rushwa.
Zaidi
ya Mainspekta wa Polisi 300 kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini
wanashiriki katika mafunzo hayo ya wiki mbili mjini Dodoma ambayo
yanafanyika kwa awamu tatu tofauti kwa lengo la kukuza maadili kwa
askari Polisi wa ngazi ya kati.
0 comments:
Post a Comment