Home » » MIRADI YA MAJI YA ZAIDI YA SH.BILLION 15 YAZINDULIWA JIJINI DAR

MIRADI YA MAJI YA ZAIDI YA SH.BILLION 15 YAZINDULIWA JIJINI DAR

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Bashir Mrindoko (katikati), akiwaeleza wafadhili wakuu wa mradi wa Maji Yetu, Eric Beaune, kutoka Umoja wa Ulaya (EU) (kushoto) na Peter Moors, kutoka Ubiligiji baada ya uzinduzi wa visima vya mradi wa maji katika shule za msingi Mbagala Kuu jijini Dar es Salaam.
Serikali kwa kushirikiana na serikali ya Ubelgiji na Umoja wa Ulaya imezindua miradi ya maji yenye thamani ya Sh. bilioni 15.7 katika  wilaya za jijini Dar es Salaam.
Miradi  hiyo ipo 15 ambayo inalenga kuwanufaisha wananchi 170,000  katika wilaya ya Ilala ambayo itakuwa na  miradi mitano, Kinondoni muradi minne na Temeke miradi sita.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Bashiru Mrindoko alisema mradi hiyo ni mkubwa na kuwataka wananchi kuitunza kwani itasaidia kwa kiwango kikubwa kutatua tatizo la maji jijini humo.

Alisema wizara yake imetengewa bajeti ya Sh. bilioni 10.7 kwa ajili ya sekta ya maji na itasaidia kutatua tatizo la maji kwa asilimia 50 jiji Dar es Salaam.

"Huu mradi wa maji ni zaidi ya bajeti yetu ya fedha tunazopatiwa hivyo ni lazima miundombinu itunzwe kwa umakini na yule atakayebainika kuhujumu atawajibishwa kwani atakuwa ana hujumu uchumi," alisema.

Aidha, alisema atalishughulikia tatizo la umeme ili kuepukana na matumizi ya diseli katika majenereta yatakayotumika katika mitambo ya maji, kwani bila hivyo watajikuta wakitumia gharama kubwa katika uendeshaji wa miradi hiyo.

Naye Balozi wa Ubelgiji nchini, Koenraad Adam alisema lengo la mradi huo ni kusaidia familia ili ziweze kuishi katika mazingira bora.

Alisema bila maji safi hakuna maisha bora kwa wananchi hivyo wananchi  wanatakiwa kusimamia viwango vya usafi na kutunza mazingira yanayoizunguka miradi hiyo.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa