Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf
Mwenda (katikati), akizungumza na Wenyeviti wa Mitaa wa Manispaa hiyo
(hawapo pichani), Dar es Salaam leo, katika mkutano wa kujadili
maendeleo na changamoto zilizopo. Kulia ni Naibu Meya, Songolo Mnyonge
na Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Manispaa hiyo, Juma Mgendwa.
Wenyeviti wa Mitaa wa Manispaa ya Kinondoni wakiwa kwenye mkutano na Meya wao, Yusuf Mwenda.

Meya Yusuf Mwenda akiteta jambo na mmoja wa wenyeviti hao baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
WENYEVITI wa Mitaa wa Manispaa ya Kinondoni wametakiwa kujituma na kuhimiza watu katika maeneo yao kulipa kodi mbalimbali zikiwemo za majengo ili kuipatia mapato Manispaa hiyo.
Mwito huo ulitolewa na Meya wa Manispaa hiyo Yusuf Mwenda wakati alipokutana na wenyeviti hao katika mkutano wa kawaida uliofanyika Dar es Salaam leo.
"Nawaombeni kujenga tabia ya kujituma na kuwahamasisha wananchi wenu katika mitaa yenu kulipa kodi mabalimbali zikiwemo za majengo" alisema Mwenda.
Aliongeza kuwa mapato yanyopatikana kutokana na kodi hizo kiasi kinarudi katika mitaa yao kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.
Akizungumzia kuhusu mkutano huo alisema lengo lake ni kupeana taarifa mbalimbali za maendeleo na kujua changamoto walizonazo ili kuzitafutia ufumbuzi wake na ajenda ya kuboresha ukusanyaji wa mapato ya Halmshauri hiyo.

0 comments:
Post a Comment