Home » » WENGI WAJIUNGA NA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI WA PSPF WAKATI WA BONANZA LA MICHEZO DAR LIVE

WENGI WAJIUNGA NA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI WA PSPF WAKATI WA BONANZA LA MICHEZO DAR LIVE

Mfuko wa Penisheni wa PSPF umedhamini Bonanza la michezo lililofanyika jumapili ya terehe 2 mwezi Machi ambapo wanamichezo wengi baada ya kupata taarifa za kutosha juu ya faida ya Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS) uliochini ya mfuko huo, wemejaza fomu na kujiunga na mpango huo ambao unawapa fursa watu wote walio kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi kujiwekea akiba na kunufaika na mafao mbalimbali.

Blogzamikoa inakuletea matukio mbalimbali katika picha kutoka kwenye bonanza hilo la aina yake lililofanyika kwenye ukumbi wa Dar Live.
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS) kutoka PSPF, Mwanjaa Sembe akikabidhi zawadi ya jezi kwa mwakilishi wa tmu ya mpira wa miguu Magenge 20 ambao wameibuka washindi wa kwanza kwenye bonanza hilo
 Wanamichezo wakiwa kwenye banda la PSPF kujiandikisha ili kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS)

 Netball inaendelea 
Afisa wa PSPF, Eliachi Remmy (kushoto) akitoa maelekezo kwa mshiriki wa bonanza hilo juu ya kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS)

Afisa wa PSPF, Amiri Issa (kulia) akitoa maelekezo kwa mshiriki wa bonanza hilo juu ya namna ya kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS)
 Mwanachama mpya katika Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS) akipiga picha ya kitambulisho chake cha uanachama muda mfupi tu baada ya kumaliza kujaza fomu za kujiunga na mpango huo wa uchangiaji wa hiari
Mafisa wa PSPF, Amiri Issa na Rose Olal (waliovaa flana za njano) wakitoa maelekezo ya namna ya kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS) kwa washiriki waliohudhuria kwenye bonanza hilo la michezo
Afisa wa PSPF, Halima Issa akielezea faida za kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS) kwa mmoja wa washiriki waliohudhuria kwenye bonanza hilo la michezo


 Bonanza hilo lilihusisha michezo mbalimbali ukiwemo huu wa kubembea
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS) kutoka PSPF, Mwanjaa Sembe akitoa maelekezo ya kujaza fomu za kujiunga na Mpango huo
 Mjumbe wa Baraza la Vijana Mkoa wa Dar es Salaam, Olivia Sanare (wa pili kutoka kulia) akikabidhi zawadi
Mwakilishi wa Global Publishers (wa pili kutoka kushoto) akitoa shukran kwa PSPF kwa kutoa udhamini kwenye bonanza hilo, wengine ni Katibu wa Klabu ya Magenge 20 Jogging, Sozigwa Kumbuka (kushoto), Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS) kutoka PSPF, Mwanjaa Sembe (wa pili kulia) na Mratibu wa Bonanza hilo Rajab Mleta

  
 Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS) kutoka PSPF, Mwanjaa Sembe akikabidhi zawadi ya jezi kwa mwakilishi wa timu ya mpira wa miguu ya Wadau




Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa