Home » » Mhadhiri ahoji: CCM wanataka nini

Mhadhiri ahoji: CCM wanataka nini

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
CCM
 
Hoja ya CCM kuwa uwepo na serikali tatu unaweza kuvunja Muungano inaweza kutafsiriwa kuwa ni  kuhofia  kugawana madaraka kwani hakuna Rais atakayekuwa na nguvu kama ilivyo sasa.
 
Mhadhiri wa Shule  Kuu ya Sheria ya  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Jesse James , alisema hayo alipoulizwa na NIPASHE kuhusu sababu za CCM kuhofia kuwa  serikali tatu zitavunja Muungano.
 
“Ninachokiona kama hoja ya CCM ambayo hawaisemi kwa kina pengine wanaogopa kugawa madaraka maana ukiwa na serikali tatu hakuna Rais atakayekuwa na nguvu kama ilivyo Rais wa sasa.” Alisema Jesse. 
 
Alifafanua kuwa  hofu hiyo pengine inatokana na uwezekano wa chama zaidi ya kimoja kushinda uchaguzi na kushika dola,hivyo inawezekana vyama vitatu vikaongoza nchi.
 
Alisema CCM mathalani naweza kushinda kwenye uchaguzi wa serikali ya Muungano, Chadema wakachukua ushindi serikali ya Tanganyika na pengine  CUF  ikashinda na kuchukua serikali Zanzibar.
 
Hata hivyo, alisema haoni sababu kwanini Muungano uvunjike na kueleza kuwa anaamini kuwa kabla ya kuuvunja wananchi wataangalia faida na hasara zake ni jambo ambalo halina haja ya kuwaletea hofu Watanzania.
 
“Pengine kama viongozi hawatakuwa na nia njema wanaweza kuleta mtafaruku na kuvunja Muungano,” alionya.   Jesse alisema  CCM walitakiwa kueleza kile wanachosema  muundo wa serikali wanaoutaka ni wa serikali mbili zilizoboreshwa.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa