Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wakati utata wa kuchotwa kwa fedha katika Akaunti ya Escrow
iliyofunguliwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutokana na mgogoro
baina ya IPTL na Tanesco ukiendelea kuzua maswali, Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema fedha hizo hazikuwa za
Serikali.
“Hizo fedha hazikuwa za Serikali, Tanesco
ilitakiwa kulipa Capacity Charge (gharama za uwekezaji) kwa IPTL kama
inavyolipa karibu Sh27 bilioni kwa kampuni nyingine zinazozalisha
umeme,” alisema Profesa Muhongo.
Itakumbukwa kuwa, kutokana na mgogoro wa IPTL na
Tanesco akaunti hiyo ilifunguliwa ili fedha ambazo Tanesco ilipaswa
kuilipa IPTL kwa ajili ya Capacity Charge ziwekwe kwenye akaunti hiyo
hadi mgogoro huo utakapomalizika.
Kwa kuwa malalamiko yalikuwa kwamba, fedha ambazo
Tanesco ilikuwa ikiilipa IPTL zilikuwa nyingi kuliko ilivyostahili,
ilitarajiwa kwamba baada ya kesi iliyofunguliwa Marekani kuamuriwa,
ingepatikana njia kukokotoa gharama halisi na sehemu ya fedha hizo
kurudi Tanesco.
Sehemu ya taarifa kwa umma iliyotolewa na Ofisi ya
Uhusiano Tanesco Makao Makuu, Jumanne iliyopita kufafanua taarifa
zilizokuwa zimeandikwa juu ya hukumu hiyo inasema: “Mahakama hiyo (ya
Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji) haikutangaza
aliyeshinda wala kushindwa.
“Ilichofanya ni kutoa muda wa miezi mitatu kwa
pande zote mbili, (Standard Charted Bank Hong Kong (SCB-HK)) na Tanesco
kwenda kukubaliana nje ya Mahakama… kwa sasa kuna mazungumzo
yanayoendelea kuhusu taratibu za kukokotoa gharama halisi.
“Hivyo basi, kanuni itakayokubaliwa na pande hizo
mbili ndiyo itakayosema SCB-HK alipwe kiasi gani ambapo ilitarajiwa
angelipwa kupitia fedha zilizokuwa Escrow.”
Profesa Muhongo alipoulizwa iwapo Serikali
inaitambua SCB- HK na hukumu iliyotolewa na Mahakama hiyo ya Kimataifa,
alisema kwa kifupi: “Kwani sisi tunaendeshwa na sheria za Marekani? Je,
hao wabia wengine wanamtambua SCB-HK?”
Pia hakutaka moja kwa moja kukiri kuwa Serikali
ndiyo iliyotoa fedha hizo na kuzitoa kwa Pan African Power Solution wala
kukanusha taarifa hizo, badala yake alisema swali hilo waulizwe
wahusika katika suala hilo.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment