Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar
es Salaam, imewasomea mashtaka matatu askari polisi watano kwa kosa la wizi wa
kutumia silaha.
Mbali
ya kuwasomea mashtaka hayo, pia imefunga dhamana askari hao ambao
wanadaiwa kushirikiana na watuhumiwa wengine kutenda makosa hayo kinyume
cha sheria.
Mbele ya Hakimu Athuman Nyamlani, wakili wa Serikali Massy Bondo, alidai Februari 17 mwaka
huu,
huko Boko Basihaya, Wilaya ya Kinondoni, washtakiwa hao walivamia Kituo
cha Mafuta GBP, kuwatishia kwa bunduki, Bi. Joyce Paulo na Bi. Diana
Wariona.
Alidai washtakiwa hao walifanikiwa kuiba pesa taslimu sh. 77,379,240 mali ya kituo hicho.
Aliwataja
washtakiwa hao kuwa ni E.6396 CPL Rajabu (39), mkazi wa Mtoni Kijichi
na F.9412 PC Saimon Chialo, mkazi wa Mtoni Kijichi.
Wengine ni F. 9414 PC Albanus, F.9521 PC Selemani (36), mkazi wa Mtoni Kijichi na Salimu Abdul, wote wakazi wa Dar es Salaam.
Bondo
aliongeza kuwa, katika tukio hilo washtakiwa ambao walishirikiana na
askari hao kufanya wizi huo ni German Chaba, ambaye ni Meneja wa kituo
hicho na Bahai Ahmed (35).
Askari hao, walipandishwa kizimbani kwa
mara ya pili na kusomewa shtaka jingine la kuiba vitu mbalimbali ikiwemo
televisheni, kompyuta mpakato na remoti ambavyo vyote ni mali ya
mlalamikaji Deogratius Ngonyani.
Kesi hiyo ilisomwa mbele ya Hakimu Suleiman Mzava na wakili wa Serikali, Tumaini Mfikwa.
Mfikwa alisema, tukio hilo walilifanya Machi 6 mwaka huu, eneo la Mbezi Beach ambapo kabla
ya kufanya wizi huo, washtakiwa hao wanadaiwa kumtishia kwa bunduki, Melis Deogratius.
Washtakiwa
hao walilikana mashtaka hayo na kurudishwa maabusu baada ya dhamana yao
kufungwa hadi Machi 28 mwaka huu na upepelezi umekamilika.
Wakati huo huo, washtakiwa hao walipandishwa kizimbani kwa mara ya tatu katika mahakama hiyo mbele ya Hakimu Benedicta Beda.
Wakili wa Serikali, Hilda Kato, alidai Machi 9 mwaka huu, Mbezi Beach, washitakiwa hao waliiba vitu mbalimbali vyenye thamani ya
sh. 4,050,000 mali ya mlalamikaji Hong Tang.
Washtakiwa
wengine waliokuwepo katika tukio hilo na askari hao ni mfanyabiashara
Juma Omary (50), mkazi wa Mbagala, Charles Hiza (37), mkazi wa Yombo
Vituka, Ally Rashidi (37),
Adamu Mkombozi (44), mkazi wa Kariakoo na Gerald Matitu (36), mkazi wa Mtoni.
Washtakiwa wote walikana shtaka hilo na kurudishwa rumande hadi Aprili 3 mwaka huu.
chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment