Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaona wakurugenzi wa kampuni
ya Njake Hotel &Tours, Jonathan Munisi na Japhet Lema wanaokabiliwa
na kesi ya wizi kwenye akaunti ya EPA, kuwa wana kesi ya kujibu katika
mashtaka yote yanayowakabili.
Katika kesi hiyo, kampuni hiyo ya Njake Hotel
& Tours inadaiwa kuchota Sh.22 bilioni kutoka akaunti hiyo kiasi
hicho cha fedha kwa madai ilirithishwa deni hilo na Kampuni ya E.Itoh ya
Japan.
Uamuzi huo ulitolewa jana na jopo la mahakimu
watatu linaloongozwa na Jaji Beatrice Mutungi baada ya kupitia ushahidi
uliotolewa na mashahidi watano walioitwa na upande wa mashtaka pamoja na
vielelezo vilivyowasilishwa kama sehemu ya ushahidi kwenye kesi hiyo.
Baada ya uamuzi huo kutolewa, washtakiwa waliiambia mahakama kuwa
watatoa utetezi wao kwa njia ya kiapo. Mshtakiwa wa kwanza aliieleza
mahakama kuwa ataita shahidi mmoja wa kumtetea huku mshtakiwa wa pili
akijitetea mwenyewe.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 27,2014 wakati
washtakiwa hao watakapoanza kutoa ushahidi wa utetezi dhidi ya mashtaka
yanayowakabili.
Aprili 13, 2011,Mfanyakazi wa Benki ya NBC, Lyson
Mwakapenda (67), akitoa ushahidi katika kesi hiyo, aliieleza Mahakama
kuwa benki hiyo, ilizirejesha fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA),
katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), baada ya kuziona kuwa ni mzigo
kufuatia kukaa nazo kwa kipindi kirefu. Mwakapenda alidai kuwa yeye
ndiye aliyesimamia malimbikizo ya fedha za EPA yaliyotokana na fedha za
kigeni zilizolipwa na wafanyabiashara walioagiza bidhaa zao kutoka nje
ya nchi.
Alidai kuwa baada ya uhaba wa fedha za kigeni,
Benki ya NBC ililazimika kufungua akaunti hiyo ya EPA. Aliendelea kudai
kuwa Benki ya NBC ilikaa na fedha hizo kwa kipindi kirefu kiasi cha
kuonekana kuwa ni mzingo na hivyo NBC iliamua kuzirejesha BoT baada ya
Hazina na BoT kukubaliana kuhusu kuhamisha fedha hizo kutoka katika
matawi ya NBC kwenda kwenye akaunti ya EPA. Alidai kuwa NBC, ilifanya
kazi hiyo kwa maelekezo kutoka BoT.
Chanzo;mwananchi
Chanzo;mwananchi
0 comments:
Post a Comment