Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » WANAWAKE WAFANYABIASHARA MASOKONI WA MPONGEZA MKURUGENZI WA EfG KWA KUTUNUKIWA TUZO YA DK.MARTIN LUTHER KING JR

WANAWAKE WAFANYABIASHARA MASOKONI WA MPONGEZA MKURUGENZI WA EfG KWA KUTUNUKIWA TUZO YA DK.MARTIN LUTHER KING JR

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Mkurugenzi Mtendaji wa asasi isiyo ya kiserikali ya Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akiwa amebeba tuzo hiyo.

Wanawake wafanyabiashara katika masoko wakiwa wamembeba Mkurugenzi Mtendaji wa asasi isiyo ya kiserikali ya Equality for Growth (EfG), Jane Magigita Dar es Salaam leo, wakati wakimpongeza kwa kutunukiwa Tuzo ya Dk. Martin Luther King aliyotunukiwa na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blaser kwa kupigania haki za kisheria za wanawake.
 Hapa wakimpokea mkurugenzi huyo kwa bashasha.


 Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo iliyokwenda sanjari na kuadhimisha siku ya wanawake duniani

Wanawake wafanyabiasha katika masoko mbalimbali ya Manispaa ya Ilala wakiwa kwenye hafla hiyo.
 
Na Dotto Mwaibale

WANAWAKE nchini wametakiwa kuelekeza nguvu zao kupinga vitendo vya ukatili wa jinsia katika maeneo wanayoishi na yale wanayofanyia kazi pamoja na masokoni.

Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa asasi isiyo ya kiserikali ya Equality for Growth (EfG), Jane Magigita Dar es Salaam leo, wakati akiwaonesha wanawake wafanyabiashara katika masoko wa soko la Tabata Muslim Tuzo ya Dk. Martin Luther King aliyotunukiwa na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blaser kwa kupigania haki za kisheria za wanawake.

"Tuzo hii niliyopata ni changamoto kubwa kwangu kwa kupigania haki za wanawake na hiyo imetokana na ushirikiano baina yangu na nyinyi hivyo tusibwete tuendelee kupigania haki zetu za kupinga ukatili wa jinsia kila sehemu tulipo" alisema Magigita.

Magigita alisema amepokea tuzo hiyo kwa niaba ya wanawake wengi wa Tanzania wanaofanyakazi katika sekta isiyo rasmi ambao wanafanyakazi zao kwenye mazingira magumu na kujinyima huku wakitoa mchango mkubwa kwa uchumi wa familia na taifa lao lakini bado wanaendelea kunyanyaswa na kuwekwa pembezoni.

"Naichukulia tuzo hii kama tuzo kwa wale ninaowahudumia, asilimia 96 ya wanawake wa kitanzania wanaopata kipato chao kupitia sekta isiyo rasmi.

Tuzo hiyo ya Haki ya Dk. Martin Luther King Jr watanzania wengine waliowahi kutunukiwa ni pamoja na Jaji mstaafu Joseph Warioba 1999, Hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere, Jaji Francis Nyalali 2002, Profesa Geofrey Mmari 2003, Justa  Mwaituka 2004, Balozi Getrude Mongella 2005.

Wengine ni Dk. Salim Salim 2006, Hayati Rashid Kawawa 2007, Regnald Mengi 2008, Dk. Malina Njelekela 2010, Jaji mstaafu Augustino Ramadhani 2012, Profesa Esther Mwaikambo 2013, Jumuia ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) 2009 na Kamati ya Watu sita ya Zanzibar iliyowezesha kura za maoni kuhusu kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa 2011.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa