Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » NLD,TADEA,NRA, CCK WJIUNGA NA CCM

NLD,TADEA,NRA, CCK WJIUNGA NA CCM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mwenyekiti wa kundi la wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wanaojiita Tanzania Kwanza Said Nkumba (watano kulia), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo yaliyojiri katika awamu ya kwanza ya vikao vya bunge mjini Dodoma jana. Wengine ni wajumbe wa umoja huo. Dk Emmanuel Nchimbi, Evod Mmanda, Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima na Suleiman Jafo.
Kamati  inayoundwa na vyama visivyokuwa na wabunge inayojitambulisha kama Tanzania Kwanza nje ya Bunge kutoka vyama vya Chausta, Tadea, NLD, Chausta, CCK, APPT-Maendeleo, Chaumma na DP, imesema itafanya maandamano kwa kushirikiana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kanda saba kuwapinga Ukawa.
Tamko hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Augustino Matefu, jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Kamati hiyo imesema kuwa itafanya hivyo ili kupinga kile walichokiita upotoshwaji unaofanywa Ukawa.

Kanda hizo ni ya Magharibi, Kusini, Nyada za Juu Kusini, Mashariki, Kaskazini, Ziwa, Unguja na Pemba.

Viongozi kutoka CCM, ambao watashirikiana na kamati hiyo, ni Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Asiyekuwa na Wizara Maalumu), Profesa Mark Mwandosya; Naibu Waziri wa Fedha (Sera), Mwigulu Nchemba naSpika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho,

Wengine ni Katibu wa Halmashauri Kuu (Nec), Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye; Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu; Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Paul Makonda; Mwenyekiti wa UVCCM, Sadifa Juma Khamisi na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid.

Mbali na maandamano, kamati hiyo imesema pia kwa kushirikiana na viongozi hao watafanya mihadhara katika maeneo hayo kuwaelimisha Watanzania dhidi ya upotoshwaji unaofanywa na Ukawa.

Alisema wamepanga kufanya hivyo kwa lengo la kuwapa wananchi uelewa juu ya mchakato mzima wa katiba ulivyoanza hadi ulipofikia na kuondoa fikra potofu zisizo na maslahi kwa taifa zinazoenezwa na Ukawa sehemu mabambali za nchi.

“Hatutaweza kuvumilia kuona watu wakiendesha mikutano, ambayo inalenga kuligawa taifa kwa kusababisha upotevu wa amani utokee, tutembea nchi nzima kutokomeza fikra mbaya zinazoendelea kupandikizwa na Ukawa,” alisema Matefu.

Aliongeza: “Tumeona baadhi ya wajumbe wasivyokuwa na mapenzi ya dhati kwa taifa, tutawaeleza wananchi wakatae sera ya serikali tatu inayoenezwa na kundi hilo kwa kuwa haina nia njema kiusalama. Inalenga kuvunja Muungano wetu.”

“Inafahamika kabisa kwamba, kuna baadhi ya Ukawa vyama vyao vinafadhiliwa na mataifa ya Ulaya Magaharibi, ambayo hayana nia njema kwetu yanawatumia hawa kupandikiza chuki miongoni mwetu na kutaka kuligawa taifa.”

Alisema kamati yake inalaani kauli zote mbaya zilizotolewa na baadhi ya wajumbe waliomo ndani ya Ukawa zilizolenga kuwakashifu na kuwachafua waasisi wa taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume bila kujali heshima waliyonayo ulimwenguni.

Alitaja ratiba ya maandamano hayo kuwa katika kanda ya Kusini yataongozwa na Kificho, Magharibi (Mwigulu na Idd Majuto), Nyanda za Juu Kusini (Profesa Mwandosya), Kaskazini (Dk. Mwakyembe), Kati (Nkumba) na Unguja (Sadifa).

Pemba (Hamad), Mashariki (Renatus Muabhi na Nape), Ziwa (Mtemvu, Makonda na Matefu).

Matefu alisema kamati yao haifungamani na upande wowote, bali inasimama kwenye misimamo na misingi yenye kuleta usawa na uzalendo iliyowekwa na waasisi wa taifa.

Alisema kinachotakiwa kufanyika sasa ni kutafauta maridhiano baina ya pande mbili hizo kwa kufanya mazungumzo yatakayoleta mwafaka utakaojenga taifa na siyo majibizano yanayoendelea yenye mpango wa kuvunja umoja na amani iliyopo nchini.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa