Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » JK KUONGOZA MASHAURIARIANO YA MRADI WA MABASI

JK KUONGOZA MASHAURIARIANO YA MRADI WA MABASI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Rais Jakaya Kikwete anatarajia kuongoza mkutano wa mashauriano ya awamu ya kwanza ya uwekezaji katika mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART) utakaowakutanisha wawekezaji wa ndani na nje Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa DART, Asteria Mlambo alisema mwishoni mwa wiki kuwa mkutano huo utakaofanyika mapema mwezi ujao utatoa nafasi kwa wawekezaji kuzijua fursa za uwekezaji zitakazopatika kwenye mradi huo.
Washiriki wa mkutano huo wanatarajiwa kutoka katika benki na taasisi mbalimbali za kifedha, kampuni za kutengeneza mabasi, kampuni za mawasiliano, mifuko ya kijamii na wengine.
Mada kuhusu mradi wenyewe wa DART itatolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Jumanne Sagini.
Kabla ya mkutano huo, DART imeandaa mkutano wa wamiliki wa daladala Dar es Salaam, Kampuni ya Usafirishaji Dar es Salaam (UDA) na wadau wengine ili kuwafahamisha jinsi gani wanaweza kunufaika na mfumo huo mpya.
“Tutawaelezea faida na fursa zitakazopatikana kwenye mfumo mpya wa usafirishaji jijini,” alisema Mlambo.
Mwezi uliopita Dart ilikamilisha shughuli ya kusajili mabasi ya daladala yanayopita katika Barabara ya Morogoro au kukatiza katika njia hiyo ikiwa ni moja ya matayarisho ya kupisha mradi huo.
Kulingana na mpango huo wa Dart barabara hizo za Morogoro, Kawawa na Msimbazi zitatumiwa na mabasi ya mfumo huo pekee kwa njia 64 Dar es Salaam zitakoma kutumika kutokana na mradi huo.
Chanzo:Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa