Home » » NANI:WAPENIWATOTO ELIMU BORA

NANI:WAPENIWATOTO ELIMU BORA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
  Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Francis Nanai (kushoto) akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya Shule ya awali ya JOMAK iliyopo Kunduchi jijini Dar es Salaam,Neillah Othman wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo jana.Kulia ni Mkurugenzi wa shule hiyo,Kavishe Kimario

Wazazi na walezi nchini wameshauriwa kuhakikisha wanawapatia elimu bora watoto wao kwa kuwa ni taifa la kesho.
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Francis Nanai alisema hayo jana alipozungumza katika mkutano wa wazazi wa Shule ya Awali ya Jomak iliyopo Bahari Beach jijini Dar es Salaam akieleza kuwa Tanzania inakabiliwa na tatizo la elimu.
Alisema kuwa uwekezaji katika elimu ni gharama kama ambavyo Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alivyowahi kutahadharisha: ‘Ukifikiri elimu ni gharama jaribu ujinga’ hivyo hakuna budi kuwekeza katika utoaji wa elimu bora.
“Wazazi na walezi nawaomba muwarithishe elimu bora watoto wenu kwani wao ndiyo taifa la kesho. Bila kufanya hivyo, tutawaandalia watoto maisha yasiyo na dira,” alisema Nanai
Aliongeza: “Kama taifa, elimu imeshuka tunahitaji kuungana na kuchagua njia sahihi ya kuwaandalia maisha ya baadaye watoto wetu kwa kuwapa elimu iliyo bora kupitia Jomak.”
Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa Shule hiyo, Caroline Kavishe alisema kuwa mtoto anastahili kupewa elimu iliyo bora tangu shule za awali ili kumjenga kujiamini, kujieleza na kuzoea mazingira yanayomzunguka.
“Dhana ya elimu bora inatakiwa kutolewa tangu shule za awali, hivyo wazazi na walezi wanatakiwa kutoa kipaumbele kwa watoto wao kwa kuwarithisha elimu iliyo bora na madhubuti,” alisema Kavishe.
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa