Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa habari TSJ katika moja ya mahafali ya chuo hicho,
Mhadhiri na Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari ch TSJ cha jijini Dar es Salaam, Suzan Ndosi alisema hayo katika mahojiano na NIPASHE.
Mwalimu Ndosi alisema, “wanachokifanya viongozi nikuwaandaa Watanzania ambao baada ya miaka mitano hakutakuwa na ajira kwani hakuna viwanda, mabenki yamebinafsishwa, waajiriwa wake ni wageni, Watanzania hawa wasio na uelewa watawekwa wapi?”alihoji na kusema wataishia kwenye kuvuta bangi na biashara ya ngono.
Aliitaka serikali kuandaa mtaala wa elimu utakaowasaidia wahitimu kujitambua pia kuwawekea mazingira yatakayowasaidia kujiari kama inavyofanyika kwa mataifa mengine.
“Serikali ilitakiwa kuweka mazingira mazuri ya kutoa elimu ikiwa ni pamoja na kuwalipa walimu mishahara kwa wakati, kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia, kujenga maabara,kutoa vyakula shuleni, nyumba za walimu na kuweka miundombinu ya kuboresha elimu si kupandisha madaraja ya ufaulu kidato cha nne na sita,” alionya. Alieleza kuwa mazingira ya kuwa na elimu bora yaanzie vijijini kuwawekea wakulima miundombinu ya usafiri, masoko pembejeo na teknolojia ili kuzalisha chakula, mazao ya biashara na ya viwandani.
Akizungumzia ujasiriamali alisema serikali haina utaratibu wa wakuelimisha wananchi kutambua fursa zilizoko suala ambalo lingewavutia Watanzania wa dayaspora kuwekeza nchini kusaidia kupunguza tatizo la ajira.
“Inabidi tuwaandalie kozi fupi za kuwafundisha …. mfumo huu ukiachwa una hatari ya kuzalisha wataalamu feki.” Mwanafunzi Hassan Abdallah wa Shule ya Sekondari Kinondoni, akizungumzia hoja za Mwalimu Ndosi, alisema hayo ni matokeo ya mitihani ya maswali mengi ya kuchagua ikiwamo hisabati, yanayowafanya wanafunzi wasitumie akili na kujishughulisha.
Anaungwa mkono na Vallerian Mgani wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) anayetaka serikali kuboresha elimu kwenye shule za ngazi zote.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment