Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Idara ya Uhamiaji kwa mara ya kwanza imewakamata
raia tisa wa Iraq, akiwamo mwanamke mmoja walioingia nchini kupitia
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es
Salaam.
Wahamiaji hao haramu waliingia nchini juzi saa 8 usiku na Ndege ya Turkish yenye namba TK0603.
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara hiyo, Tatu Burhan, alisema wahamiaji hao baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina, walibainika kutumia hati mbili za kusafiria zenye uraia wa nchi tofauti lakini jina likitumika moja.
Kadhalika alisema idara hiyo imeshtushwa na kundi hilo kwa sababu haijui dhamira ya wahamiaji hao licha ya kudai kutumia njia ya Tanzania kuingia Bara la Ulaya.
Burhan, alisema idara hiyo kwa sasa iko katika mchakato kabambe wa kuhakikisha wahamiaji hao wanarudi nchini kwao kupitia ndege walioingia nayo.
Alifafanua kuwa wahamiaji hao watatu waliingia kwa hati ya kusafiria ya Iraq moja kwa moja na kutumia majina yao halisi, ila wengine walitumia hati ya kusafiria yenye uraia kutoka nchi ya Sweden, na Ubelgiji.
Aidha alisema wahamiaji walioingia nchini kupitia Uturuki ni Adel Shahalan Mohan, Osama Zaid Ghayeb na Ali Mohammed Abduli ambao walitumia hati na majina yao halisi yakiwatambulisha kama raia wa Iraq.
Aliwataja wengine ambao majina yao halisi yakiwa kwenye mabano ni Samer Helmi Sweden (jina halisi ni Lazim Mosa Hitteer), Davi Gabriel Populete (Ayad Sami Maktoof), Fawadhi Mohammed Ali (Ali Hussen Olewi), Scaden Al Khaler na Ali Oleine ( Al Mosaw Jafrad).
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment