Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Gari la kikosi cha Zima moto likiwa katika
msikiti wa Mtambani katika harakati za kuzima moto huo iliowaka majira
ya saa moja usiku jana
Tukio hilo limetokea jana majira ya jioni na kusababisha mamia ya wananchi kujitokeza kusaidia kuuzima kabla ya vikosi vya zima moto kuwasili eneo la tukio.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo baada ya kuzungumza na NIPASHE akiwa eneo la tukio.
Hata hivyo, chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana na hadi tunakwenda mitamboni, vikosi mbalimbali vya zimamoto kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam vilikuwa vikiendelea kuuzima moto huo.
Msikiti huo pia una shule za sekondari na msingi za Mivumoni.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment