Home » » MFANYA BIASHARA ADAKWA NA MACHINE 'FEKI' EFD

MFANYA BIASHARA ADAKWA NA MACHINE 'FEKI' EFD

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba
 
Serikali kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi limemkamata mfanyabiasha jijini Dar es Salaam na mashine ‘feki’ ya kutolea stakabadhi ya EFD, ambazo ziliibwa mkoani Mwanza.
Alikamatwa katika operesheni iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana ikiongozwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, kwa kushirikiana na maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mfanyabiashara aliyekamatwa na mashine hiyo yenye namba 031TZ 54000053 ni Mkurugenzi Kampuni ya Uchapishaji ya Fasad Nasoro anayemiliki Kampuni ya CI Group ya jijini Dar es Salaam.

Nasoro alisema mashine hiyo aliuziwa na kampuni ya wakala ya kutoa mashine hizo ya jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu ya Waziri Nchemba, serikali imefuatilia kwa muda na kufanya uchunguzi na kugundua kuwa mashine hiyo ilitoa stakabadhi feki kwa kampuni kubwa nchini.Alisema mabilioni ya shilingi yamepotea na kuikosesha serikali mapato.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa