Home » » HOFU YA EBOLA DAR, MGENI KUTOKA BENIN ALAZWA TEMEKE

HOFU YA EBOLA DAR, MGENI KUTOKA BENIN ALAZWA TEMEKE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Watu wakikatiza kwenye lango la kuingilia katika Hospital ya Temeke, sehemu ambayo anayedaiwa kuwa mgonjwa wa Ebola amelazwa  
 Hofu ya ugonjwa wa ebola imeingia jijini Dar es Salam baada ya msichana anayedhaniwa kuwa na ugonjwa huo kutua nchini akitokea Benin, Afrika Magharibi na kulazwa katika Hospitali ya Temeke.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Amani Malima alithibitisha kuwapo msichana huyo mwenye umri wa miaka 14 aliyeingia nchini jana kuonekana akiwa na dalili hizo.
“Huko alikotoka alihisiwa kuwa na dalili hizo, alipofika hapa madaktari walipomhoji alisema ana maumivu makali ya viungo, miguu na mikono,” alisema.
Dk Malima alisema baada ya kupata maelezo hayo, walichukua vipimo vyote vya damu na majibu yake yatatoka leo kujua kama ana ugonjwa huo au la.
“Tumegundua kwamba ana malaria lakini vipimo vya ebola majibu ni kesho (leo), hivyo tunaangalia namna ya kumtibu na kama atakuwa hana ugonjwa huo tutamruhusu,” alisema Dk Malima.
 Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa