Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbunge wa Kongwa, ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai
Ndugai aliliambia NIPASHE jana kuwa kwa miaka 15 aliyotumikia
jimbo hilo kama mbunge, amefanikisha kupatikana kwa maendeleo na kwamba
anaamini wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 hatakabiliwa na ushindani
wa aina yoyote.
“Nina hakika mwakani hakuna atakayechukua fomu hapa, lakini
nikimaliza awamu ijayo, sitagombea tena,” alieleza Ndugai huku
akionyesha kujiamini.
Alipotakiwa kueleza ikiwa nia yake ya kutogombea tena iwapo atapata
na kumaliza kutumikia kipindi hicho, inatokana na mabadiliko ya Katiba
ambayo mchakato wake unaendelea, Ndugai alisema hiyo siyo sababu.
Alisema miaka 20 na itatosha kuwaachia wengine wenye uwezo na nia ya kutumikia umma.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment