Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura
Vurugu hizo zilizopelekea bajaj mbili kupasuliwa vioo na dereva
mmoja wa bajaji kujeruhiwa, zilizotokea Kimara Mavurunza katika kituo
cha daladala cha Baa mpya.
Aidha, hali hiyo imepelekea baadhi ya madereva wa daladala kushikiliwa katika kituo cha polisi Mbezi Kimara.
Kwa miaka kadhaa kumekuwapo na shida ya usafiri kwa kwa abiria
watokao Kimara Mwisho kuelekea Kimara Bonyokwa kutokana na njia kuwa
mbaya, hali inayo changia wamiliki wa vyombo vya abiria kushindwa
kupeleke vyombo vyao katika maeneo hayo.
Kutokana na hali hiyo, baadhi ya daladala zisizo kuwa na vibali vya
kutembea barabarani, ndizo zimekuwa zikisafirisha abiria kutoka Kimara
Mwisho kuelekea Bonyokwa.
Hivi karibuni bajaj zimeanza kutoa huduma za kusafirisha abiria
kutoka Kimara-Bonyokwa kwa nauli ya Sh. 1,000 na kusababisha baadhi ya
madereva wengi wa daladala kuwafanyia vurugu wenye bajaj.
Mwenyekiti wa madereva bajaj Kimara, John Muhuni, alisema fujo hizo
zilisababishwa na madereva wa daladala kujifanya kuwa wao ndio wenye
njia hiyo.
“Tumeanza kubeba abiria hapa huu ni mwaka wa pili, kila wakati
wamekuwa wakitufanyia fujo, tunafikisha taarifa polisi, lakini hakuna
hatua zinazochukuliwa,”alisema Muhuni.
Aliongeza kuwa baada ya kuona hivyo waliamua kupeleka taarifa
katika uongozi wa serikali za mitaa na juzi waliamua kuwakutanisha.
Muhuni aliongeza baada ya kukutana walikubaliana kila mtu apakie abiria kupeleka katika kituo cha Baa Mpya.
“Lakini toka jana (juzi),wenzetu wamekuwa wakijiandaa kutufanyia fujo,”alisema.
Jacqueline Makalu, Makamu Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa ya Kimara
Bonyokwa alisema fujo hizo zilianza saa 1:00 asubuhi na kumalizika saa
3:00 asubuhi baada ya polisi kuwasili.
Aliongeza kuwa madereva wa daladala wamekuwa wakorofi kwa muda mrefu na kwamba kwa sasa wamewawekea sheria ambayo itawadhibiti.
Dereva wa daladala, Kasimu Masumbuko, alisema wamekuwa wakiwaomba
bajaj kuacha kupakia abiria kwa,kuwa wanawachukulia wateja wao, lakini
wenzao wanawapuuza.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura,
alidhibitisha kutokea kwa tukio hilo huku na kusema uchunguzi
unaendelea kubaini wahusika.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment