Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira, imeandaa mpango wa kutoa
elimu kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali, ili kuwajenga wasomee fani zenye
fursa za ajira.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa
Habari Mkuu wa Sekretarieti ya Ajira, Riziki Abraham alisema mkakati huo
unalenga kupunguza tatizo la ajira.
“Ukweli ni kwamba, ajira zimekuwa za ushindani kwa
sababu vyuo vimekuwa vingi, lakini kuna programu tumeanzisha ya
kuwahamasisha wanafunzi kutojenga dhana ya kuajiriwa pekee au
kung’ang’ania fani zisizokuwa na soko,” alisema Abraham na kuongeza:
“Sisi kazi yetu ni kuwashauri, hivyo chini ya programu hii tunalenga
kuwashawishi wasome kulingana na mahitaji ya soko la ajira.”
Pia alitumia fursa hiyo kuwaonya watumishi wa
umma, hasa wanawake ambao wamekuwa na tabia ya kubadilisha majina
kiholela pindi wanapoolewa.
“Sekretarieti ya Ajira, inawataka wote waliobadili
majina kwa sababu mbalimbali iwe ya kidini, kuolewa au kutopenda yale
ya utotoni na kuwa na majina tofauti kwenye vyeti, wafuate sheria,”
alisisitiza.
Alifafanua kuwa siyo vibaya kwa mwanamke kubadili
jina na kutumia jina la ubini wa mumewe, ingawa pia wapo ambapo
wamejikuta katika wakati mgumu baada ya ndoa zao kuvunjika, hivyo
kuhangaika kubadilisha majina kwa mara nyingine.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment