Home » » KITUO CHA DALADALA DAR KUFUNGULIWA LEO

KITUO CHA DALADALA DAR KUFUNGULIWA LEO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Kituo cha daladala cha Simu 2000 kinatarajia kuzinduliwa leo baada ya maandalizi na taratibu za kukifungua kukamilika.

NIPASHE jana lilifika katika kituo hicho na kushuhudia mafundi wakimalizia kazi ndogondogo zikiwamo kukarabati mabomba ya kupitishia maji ya mvua na eneo la wafanyabiashara.

Baadhi ya abiria walisema wanafurahishwa na hatua hiyo ya kuhamishia kituo cha Ubungo katika eneo hilo, kwani walikuwa wapata adha kubwa wakati wa kupanda daladala kutokana na kukosekana kwa eneo maalumu la kupandia daladala zote.

Shamimu Kigomba, mkazi wa Kimara, alisema baada ya kituo cha awali kufungwa kutokana na ujenzi wa barabara wa mabasi ya mwendo haraka  (Darts), walikuwa wakipata shida kutafuta usafiri kutokana na kukosekana eneo rasmi la kupaki daladala.

“Mimi naona ni vyema kwani tunapata shida sana, ukitaka kushuka Ubungo utafute gari nyingine, ni lazima utembee umbali mrefu, magari mengi na foleni zilizotokana na magari kushusha abiria barabarani,” alisema. Aron Kika, mkazi wa Tabata, alisema kituo hicho kitarahisisha usafiri kwani kwa muda mrefu watu walikuwa wakikosa muelekeo kutokana na kukosekana kwa kituo rasmi cha abiria.

 “Sawa sisi tutaenda ila serikali inapaswa ihakikishe inamalizia lile eneo la lami lililobaki na siyo kuacha vile siku tatu unakuta barabara imeharibika, kama ambavyo wamejenga kituo cha makumbusho bila kukarabati barabara za kuingilia,” alisema Salehe Kisele, dereva wa daladala yza Mbezi Makumbusho.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa