Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » SH. BILIONI 10 ZAHITAJIKA KWA MADAWATI SHULE ZA DAR

SH. BILIONI 10 ZAHITAJIKA KWA MADAWATI SHULE ZA DAR

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki.

Serikali imesema inahitaji Sh. bilioni 10 kumaliza tatizo la madawati linazozikabili shule mbalimbali za msingi na sekondari jijini Dar es Salaam.

Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 44.4 ya shule za kata zilizoko nchini zinakabiliwa na upungufu wa madawati, tatiazo hilo limechangia kati ya watoto 10 wanaokwenda shule nusu yake wanakaa chini.

Pia, kwa mkoa wa Dar es Salaam pekee shule za msingi zinahitaji madawati 67,000, tatizo hilo limetoa msukumo kwa serikali kushirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), kuwashirikisha wadau kuangalia njia mbadala ya kutatua.

Akipokea msaada wa madawati 1000 kutoka kwa Kampuni ya Total Tanzania Limited, kwa kushirikiana na Social Action Trust Fund   (SATF), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, alisema serikali imebaini ongezeko kubwa la Watanzania waishio hapo ndilo linalochangia tatizo hilo.

Alisema takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 10 ya Watanzania wanakimbia mikoani kwenda kuanzisha maisha Dar es Salaam huku idadi ya kuzaliana ikiongezeka kwa kasi.


Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Rosemary Lulabuka, alisema msaada huo umekuja kwa wakati mwafaka na kuwa serikali imeelemewa na idadi kubwa ya shule zinazohitaji madawati hayo.

Madawati hayo yamegharimu Sh. bilioni 80 na shule 10 za Dar es Salaam zitanufaika na madawati hayo huku zoezi hilo likiendelea.

Shule hizo kwa mkoa wa Temeke ni Shule ya Msingi Chamazi, Mbande, na Kingugi. Kwa Kinondoni ni King’ong’o, Goba, Boko National Housing,  Bwawani na Bunju A wakati  Ilala ni  Hekima, Kombo.
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa