Home » » SHERIA YA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KUREKEBISHWA

SHERIA YA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KUREKEBISHWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati), akikagua jengo la Mahakama ya Mafunzo katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania, jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Naibu wake, Angellah Jasmine Kairuki na kulia ni Mkuu wa taasisi hiyo, Jaji Dk. 


Serikali imeahidi kuifanyia marekebisho sheria yamikopo itakayosimamia mikopo kwa wanafunzi  wa vyuo vikuu nchini kikiwamo Chuo cha Sheria Tanzania (IJA), ili kupanua fursa za masomo kwa Watanzania.

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea majengo ya Ija Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro,  alisema muswada wa sheria hiyo unatarajiwa kupitishwa rasmi Bungeni Novemba mwaka huu.

Alisema katika bajeti ya serikali Ija hakikuwa katika orodha ya mikopo endelevu kama vinavyopewa vyuo vingine, hivyo maboresho ya sheria hiyo yatalenga muendelezo wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wote kwani baadhi yao wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na rasilimali fedha.

Alisema mchakato wa kubadilisha sheria utakamilika rasmi 2016, baada ya serikali kukamilisha taratibu zake, na itawasaidia kundokana na misukosuko waliyokuwa wakiipitia wanavyuo wa awali.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ija, George Masaju, alisema changamoto kubwa inayowakabili wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini ni rasilimali fedha kupitia  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya  Juu (HELSB).
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa