Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » SHIBUDA AHUSISHWA NA TADEA

SHIBUDA AHUSISHWA NA TADEA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama cha Tadea, Joachim Mwingira (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kumtaka Msajili wa Vyama vya Siasa kuingilia kati taratibu 


Baadhi ya wanachama wa chama cha DemocraticAlliance  (Tadea), wameutuhumu uongozi wa chama hicho kutumiwa na vyama vya siasa akiwamo Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda (Chadema), kwa maslahi binafsi.

Tuhuma hizo zimetolewa na Joachim Mwingira, Makamu wa Rais Mstafu wa Tadea,Vurugu Luziga;  Katibu wa Tadea Meatu na Bavi Mdumrua, mwanachama namba 0026 wa Tadea,walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.

Walidai uongozi huo umekiuka misingi ya chama,kwa kuunga mkono uchakachuaji wa Rasimu ya iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na JajiJoseph Warioba.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Joachim Mwingira alisema chama hicho tangu wakati wa muasisi wa chama hicho, Oscar Kambona, kilikuwa na misingi ya kutetea wananchi, lakini Rais wa sasa, John Chipaka, amekuwa akienda kinyume.

Mwingira alidai kuwa Shibuda amekuwa akidhamini baadhi ya vikao vya chama hicho kwa kulipa kumbi za mikutano na posho za wajumbe wanaohudhuria mikutano.

Hata hivyo, John Shibuda alipoulizwa alisema: “Mimi ni star (nyota), siwezi kutafuta chama cha kugombea, ila mimi natafutwa na chama, mimi ni sawa na Christian Ronaldo timu zinakuja kunisajili, hao wanaosema hivyo wanababaika,” alisema Shibuda.

Chipaka alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo, alisema yuko safarini mjini Dodoma na kwamba wanachama hao hawajui.
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa